23 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

UN yakutana na wazee Tanzania kutokomeza mimba, ukatili

Benjamin Masese -Mwanza

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Masuala ya Wanawake (UN  Women),  limewakutanisha wazee 225 maarufu wa mila kutoka mikoa  tisa ikiwa ni sehemu ya kuisaidia Serikali ya Tanzania  kutimiza malengo ya mikataba ya kimataifa na kikanda  ya kukomesha vitendo ukatili wa jinsia na kuleta usawa ndani ya jamii.

Akizungumza wakati wa  ufunguzi wa semina kwa wazee hao waliokutanishwa jijini Mwanza, Ofisa Elimu na Uhamasishaji kutoka UN Women, Lucy Tesha alisema  wadau wakubwa wa mashirika ya kimataifa ni Serikali ambapo kwa pamoja hushirikiana katika masuala ambayo yamewekwa katika mikakati ya kimaendeleo kwa  kuwafikia walengwa ambao ni  wananchi.

Tesha alisema suala la ukatili wa kijinsia, mimba kwa wanafunzi na ndoa za utotoni zimekuwa  jambo kubwa ndani ya jamii  ambapo sababu kubwa zinazochangia uwepo wa mambo hayo ni baadhi ya mila na desturi  za makabila mbalimbali.

“Kama shirika ;la UN Women ambayo tunashughulika na masuala ya wanawake, tumeona kuna haja ya kuisaidia Serikali ya Tanzania kutokomeza vitendo vya mimba za wanafunzi, ukatili wa jinsia na ndoa za utotoni, sote tunajua kila nchi imekuwa na mikakati yao  ya ndani, pia  yapo malengo ya kimataifa.

“Kwa Tanzania tunataka kuona wanawake wanachangia maendeleo ndani ya familia na sio tu wanaume pekee, hapa  tunao wazee 225  tuliowakutanisha kutoka mikoa ya Mwanza, Tabora, Mara, Simiyu, Kagera, Shinyanga, Katavi, Geita na Manyara  ambapo kila mmoja atatueleza mila na desturi zao, tutajadiliana na kuona zipi zinafaa na zipi hazifai na kuwashauri kuachana nazo.

“Kama UN Women tunataka kuona wazee hawa wawe muhimili wa  ndani ya jamii katika kubadilisha fikra za wengine ili wanawake wapate usawa, mimba za kwa wanafunzi ziishe na ndoa za utoto zisiwepo tena, hatuhitaji kisikia tena ramli  changanishi zinaendelea tena,”alisema.

 Hata hivyo takwimu za 2015/2016 zilizowasilishwa  katika semina hiyo  kutoka Ofisi ya Takwimu  nchini (NBS)  zimeonyesha  mikoa inayoongoza kwa  vitendo vya ukatili ni  Mara na Shinyanga  zikiwa na asilimia 78,  Tabora 71, Kagera 67, Geita 63, Simiyu 62, Kigoma61, Mwanza 60, Njombe53, Dodoma  na Katavi 50.

Mikoa  mitatu inayoongoza kwa ndoa za  utotoni ni Shinyanga asiliamia 59, Tabora 58 na Mara 54 ambapo  mikoa inayoongoza kwa mimba za shuleni ni Katavi asilimia45, Tabora 43, Dodoma 39, Morogoro 39,Mara na Shinyanga zikiwa na asilimia 37.

Alisema shirika hilo limeamua kujikita kwa wazee hao kwa kuwa asilimia kubwa ya jamii bado inawaamini  hivyo ni rahisi kupeleka elimu katika maeneo wanayoishi kwa lengo la kutokomeza  ukatili, ndoa za utotoni na mimba kwa wanafunzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles