23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

UN yaitisha mkutano kuhusu suluhu ya kifedha kukabili Covid-19

NEW YORK

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau na Waziri Mkuu wa Jamaica, Andrew Holness wameitisha mkutano wa pamoja na viongozi wa dunia, Mashirika ya Kimataifa katika mpango jumuishi wa kukabiliana na madhara ya kibinadamu na kiuchumi ya Covid-19.

Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha viongozi wa nchi na serikali zaidi ya 50 na ni muhimu wa kusaka suluhu ya fedha kwa maendeleo ya kukabili Covid-19.

Vilevile utaangazia maeneo sita muhimu ya kufanyia kazi ili kuhamasisha uchangishaji unaohitajika kukabiliana na kupata unafuu. 

Maeneo hayo yanajumuisha kutanua uwezo wa ununuzi katika uchumi wa dunia, kukabiliana na madeni yaliyopindukia, kuzuia mtiririko wa wa fedha haramu, kuongeza uwekezaji ili kujikuza zaidi ndani na kutengeneza ajira na kuunda mfumo wa mataifa kuimarika kwa haraka zaidi, kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, kukabili mabadiliko ya tabia nchi na kurejesha ulinganifu kati ya uchumi na asili. 

“Janga hili limeonyesha wazi tulivo katika hali tete, tupo katika janga la kibinadamu lisilo la kawaida kutokana na virusi visivyoonekana kwa macho tunahitajika kukabiliana nalo kwa umoja na ushirikiano na jambo muhimu la mshikamano ni msaada wa kifedha,”alisema Katibu Mkuu wa UN. 

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamaica Andrew Holness, alisema: “Janga hili la Covid-19 linatuhitaji kwamba tuchukue hatua za haraka kukabiliana na madhara yake kwenye uchumi wa mataifa yote, katika kila ukanda wa dunia na kila hatua ya maendeleo,”.

Aidha Holness alisema anakubaliana na maeneo yote sita muhimu yaliyoangaziwa kuwa yenye umuhimu wa kutazama, kutanua uwezo wa ununuzi katika uchumi wa dunia hususani kwa mataifa ya kipato cha chini na cha kati. 

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, alisema: “Mataifa yote duniani yameguswa na janga la Covid-19 na hata kutishia kudidimiza hatua ya maendeleo iliyokuwa imefikiwa.

“Tunajua njia bora ya kuwasaidia watu wetu na kujenga upya uchumi ni kwa kushirikiana kama jumuiya ya kimataifa, tunahitajika kusaidia hatua jumuishi na za mmoja mmoja kuwezesha unafuu wa ujumla, ustahimilivu wa kudumu ambapo hakuna wa kuachwa nyuma.” 

MAENEO 6 MUHIMU YA KUANGAZIWA 

Maeneo sita muhimu za kuzingatia ni hitaji la kujenga ukwasi katika uchumi wa dunia na kudumisha uimara wa kifedha na kulinda faida za maendeleo. 

Pili ni haja ya kushughulikia uelemewaji wa madeni kwa nchi zote zinazoendelea kuokoa maisha kwa mabilioni ya watu ulimwenguni. 

Tatu ni haja ya kuunda mfumo ambao wadau wa sekta binafsi wanaweza kushiriki kikamilifu katika suluhisho bora na kwa wakati unaofaa. 

Nne, juhudi za awali za kuongeza uwekezaji na malipo ya ukuaji wa pamoja na kutengeneza nafasi za ajira. 

Tano, hatua za kuongeza matumizi sahihi ya fedha na kukuza uhamasishaji wa rasilimali za ndani kwa kuzuia mtiririko wa fedha haramu. 

Sita, kuhakikisha ahueni endelevu inapatikana kwa umoja kwa kuambatanisha Sera na Malengo ya Maendeleo Endelevu. 

Takwimu za Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) zinaonesha kuwa tayari ugonjwa wa Covid-19 umechukua maisha ya watu 34,0000 na zaidi ya visa milioni 5.4 vimeripotiwa duniani.

Endapo hatua haitachukuliwwa UN imetabiri kuwa huenda ukapoteza karibu Dola za Kimarekani Trilioni 8.5 kutoka katika uchumi wa dunia katika kipindi cha miaka miwili ijayo, huku ukiwaacha watu milioni 34 katika umasikini wa kupindukia kwa mwaka huu na wengine zaidi ya milioni 130 kwenye huu muongo. 

Kuanguka kwa biashara tayari kumeshaanza kusababisha watu kupoteza ajira zao, Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) limesema huenda makadirio ya muda wa kufanya kazi katika robo ya pili ya mwaka 2020 itakuwa asilimia 10.5 chini zaidi ya kabla ya janga ambalo ni sawa sawa na kazi za kudumu milioni 305.

Hata kabla ya mlipuko wa janga hili, karibu nusu ya nchi zote zinazoendelea na nyingine zenye uchumi duni zilikaribia au kulemewa kabisa kwa madeni. 

Gharama za ulipaji wa deni kwa nchi hizo umeongezeka kwa zaidi ya mara mbili kati ya 2000 na 2019, hadi kufikia asilimia 13 ya mapato ya serikali na kufikia zaidi ya asilimia 40 katika robo ya nchi zote zinazoendelea za visiwa kidogo (SIDS). 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles