29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

UN yahitaji msaada wa dharura kukabiliana na Ebola DRC


KINSHASA, Congo DRC

TAARIFA kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kumekuwa na matukio makubwa kadhaa ya uvunjifu wa amani ambayo yameyumbisha juhudi zote za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika Jimbo la  Butembo na maeneo ya vituo vya afya yalioko jirani wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa msemaji wa UN,  Farhan Haq wakati operesheni zikiwa zimezinduliwa upya mwishoni mwa wiki iliyopita, WHO inamatumaini kwamba harakati za kuchukuwa vipimo katika maabara ambazo bado zinakabiliwa na vizuizi, vitasababisha  kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wenye virusi vya Ebola katika siku zijazo.

Msemaji huyo alisema mlipuko huu uko katika hatua hatarishi, ambako kunaongezeko la maambukizi katika wiki za hivi karibuni jambo ambalo linahatarisha kuenea kwa maambukizi hayo katika majimbo mengine nchini hapa  na nchi jirani.

Kwa upande wake maofisa wa WHO wanasema kunahitajika msukumo mkubwa wa msaada wa kisiasa na kifedha kutoka kwa wahusika nchini na Kimataifa kukabiliana na hali hiyo tata.

Walisema kuwa pengo la fedha liliopo hivi sasa linaweza kusababisha  WHO na washirika wake kusitisha baadhi ya shughuli ambazo  zinahitajika sana.

Maofisa hao walisema kuwa hadi Mei 2 mwaka huu, WHO ilikuwa tayari imepokea dola za Marekani milioni 32.5 zilizokuwa zinahitajika kuendeleza juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo kwa kiwango kilichofikiwa hivi sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles