26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UN: Somalia inahitaji msaada dola bilioni moja

New York, Marekani

UMOJA wa Mataifa (UN) umetangaza kuwa Somalia inahitaji msaada wa zaidi ya dola bilioni moja kwa huduma za kibinadamu kwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOM), fedha hizo ni za kuwasaidia watu zaidi ya milioni tatu kwa mahitaji ya msingi ya kibinadamu.

Akizungumza baada ya kuzindua wito huo wa msaada uliofanyika mjini Mogadishu, Somalia, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UN nchini humo, Adam Abdelmoula  alisema Somalia bado inaendelea kukabiliwa na matatizo makubwa ya kibinadamu.

Aliongeza kuwa miezi michache tu iliyopita watu zaidi ya nusu milioni waliathirika na mafuriko ambayo yalikumba sehemu kubwa ya Somalia.

Uzinduzi huo wa Mpango wa Kukabiliana na Masuala ya Kibinadamu (HRP) wa jumla ya Dola bilioni 1.03 umehudhuriwa pia na Waziri wa Somalia wa masuala ya kibinadamu na udhibiti wa majanga, Hamza Said Hamza aliyesema mpango huu unaashiria azma ya jamii ya kimataifa katika kuwasaidia watu wa Somalia.

Aliongeza kuwa mgogoro wa kibinadamu Somalia unachangiwa na vita ya miaka mingi, ukame wa muda mrefu na bila shaka mafuriko yaliyoshuhudiwa mwaka jana.

Fedha hizo za mpango wa HPR zitasaidia watu milioni tatu wakiwemo milioni 1.7 waliotawanywa na vita, kutokuwepo usalama, kuhamishwa kwa nguvu, ukame na mafuriko na msaada utakuwa katika mfumo wa mgao wa chakula, elimu, huduma za afya, maji safi na salama na pia ulinzi kwa walio katika hatari ya ukatili wa kijinsia.

UNSOM imesema mwaka huu mahitaji ya ufadhili ya mpango wa usaidizi wa kibinadamu yamepungua kwa asilimia 11 kutoka dola bilioni 1.08 hadi dola bilioni 1.03.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles