27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

UN: Kampuni za silaha zinachochea vita

 Riek Machar
Riek Machar

JUBA, SUDAN KUSINI

JOPO la Umoja wa Mataifa limepata ushahidi wa kuwepo mitandao ya silaha yenye makazi yake nchini Israel na barani Ulaya Mashariki ambayo inachochea vita inayoendelea sasa huko Sudan Kusini.

Wataalamu wameeleza katika ripoti yao kwenye Baraza la Usalama la umoja huo kuwa, mitandao ya uuzaji silaha kutoka Bulgaria na Israel inachochea vita nchini Sudan Kusini kwa kuwapatia waasi silaha katika nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.

Ripoti hiyo ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, ushahidi huo umefafanua kuhusu mitandao hiyo iliyojiimarisha vyema ambapo mauzo ya silaha huratibiwa kutoka kampuni za kutengeneza silaha huko Ulaya Mashariki na Mashariki ya Kati na kusafirishwa kupitia mawakala wao mashariki mwa Afrika hadi Sudan Kusini.

Wameongeza kuwa, askari watiifu kwa kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini na makamu wa rais wa nchi hiyo, Riek Machar, hivi karibuni walionekana huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa na silaha za automatiki zilizotengenezwa Israel.

Silaha hizo zilikuwa ni sehemu ya silaha zilizouzwa kwa Uganda mwaka 2007. Mapigano ya ndani Sudan Kusini yamesababisha vifo vya malaki ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles