27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ummy Mwalimu akutana na wadau wa afya kuijadili corona

Mwandishi wetu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya  mazungumzo na wadau wa sekta ya afya kwa lengo la kujadili kwa pamoja tishio la mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Waziri Ummy amesema kikao hicho waliwaeleza wadau kama taarifa ya shirika la afya duniani(WHO) ilivyotangaza hali ya maambukizi ya ugonjwa huo duniani hivyo kama serikali ni vyema kuwapatia taarifa wadau hao

“Tumewapa taarifa wadau wetu na kuwahakikishia kwamba Tanzania hakuna mtu mwenye maambukizi mwenye maambukizi ya virusi wa corona na tumewaeleza hatua gani kama serikali tumezichukua katika kujiandaa kukabiliana na tishio hili”.

Katika kikao hicho waziri ameeleza kwamba wizara yake imeweza kuchukua hatua ya kukabiliana na tishio hilo kwa kuimarisha ufuatiliaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye viwanja vya ndege na viingilio vingine ikiwemo bandarini.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kwamba wameweza kutoa mafunzo kwa baadhi ya wataalamu wa afya waliopo mikoani pamoja na kuandaa dawa, vifaa na vifaa  tiba endapo nchi itapata mshukiwa wa virusi vya corana.

“Tumewaomba washirikiane nasi katika kuhakikisha kwamba sasa tunakuwa tayari kukabiliana na tishio hilo hata kama hatuna mgonjwa hii tulikuabaliana kwenye mkutano wa nchi wanachama wa SADC kwamba nchi zote tunaingia kwenye hatua ya kukabiliana,”. amesema Waziri Ummy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles