24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UMEME STIEGLER’S GORGE WAIVA

Na BAKARI KIMWANGA-MOROGORO                |                 


NDOTO ya Rais Dk. John Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda, inaelekea kutimia baada ya timu ya mawaziri na makatibu wakuu wa wizara 14 ambazo zinatekeleza mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge kutembelea eneo la mradi huo.

Viongozi hao wameshuhudia kasi ya ujenzi wa mradi huo ambao ni mkubwa kwa historia ya Tanzania, unaotarajiwa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.

Akitoa maelezo kwa kamati ya viongozi hao, Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco – ETDCO, Mhandisi Elangwa Abubakar, alisema kwa sasa kazi ya ujenzi inayoendelea ni kusimika nyaya maalumu zenye madini ya kopa kutoka katika kituo cha Matambwe hadi eneo la mradi.

Alisema kwa ukubwa wa mradi huo, nguzo zitakazotumika mara ya kwanza ni za zege ambazo zitakuwa zaidi ya 700.

“Mradi mzima utakuwa na nguzo za zege 700 zenye urefu wa milimita 17. Na huu ni mradi wa kwanza kutumia nguzo za aina hii.

“Tunaendelea na ujenzi huu huku tukiwa tumezingatia masharti ya kitaalamu, ikiwamo kukata miti bila kuathiri mazingira kutoka usawa wa ndege.

“Kwa sasa kazi inayoendelea mafundi wanalaza kebo ambayo itazunguka na kupita chini ya reli na daraja.

“Awamu ya pili itakuwa kama ya ujenzi. Pia tutaweka kebo. Hii line itabeba 33 KV na ya pili nayo itakuwa na ukubwa kama huo, ambayo ndani yake kuna waya wa kopa pamoja na nyaya zake ambazo ni nzito,” alisema Mhandisi Elangwa.

Kwa upande wake, mjumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi huo, Mhandisi Justus Mtolera, alisema ujenzi wa bwawa la umeme utakuwa na mashine tisa ambazo kila moja ina uwezo kuzalisha megawati 235.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles