UMBO LAMKWAMISHA AKI KUCHEZA KIKAPU

0
552

 

 

 

 

LAGOS, NIGERIA


Staa wa filamu za vichekesho za Nollywood, Aki, amesema kimo chake kifupi kinamfanya ashindwe kucheza kikapu licha ya kuupenda mno mchezo huo.

Aki alisema hata hivyo hauchukii ufupi kwani haumzuii kuwa na akili nyingi alizonazo sasa.

“Nina akili sana, hivyo suala la kimo haliniumizi kichwa…nafurahia nilivyo,” alisema Aki na kuongeza kuwa hata soka amekuwa akilifuatilia.

“Mimi ni shabiki mkubwa wa Arsenal na Enyimba FC. Baba yangu alikuwa mwanasoka na hata mimi naweza kucheza,” alidai nyota huyo.

Kufikia mwaka jana, jarida maarufu la Forbes la Marekani lilidai kuwa mwigizaji huyo ana utajiri wa zaidi ya Dola milioni 3.5 (zaidi ya Sh bilioni 7 za Tanzania).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here