23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ulijua nyuma ya Niyonzima mpya yupo Adel Zrane?

MWAMVITA MTANDA

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya ili mfululizo.

Mafanikio ya Simba yametokana na sababu nyingi, ikiwemo ukubwa au  upana wa kikosi hicho, mbinu pamoja na ufundi wa benchi la ufundi la timu hiyo linaloongoza na kocha mbelgiji, Patrick Aussems na ubora wa  mchezaji mmoja mmoja.

Ninapozungumzia ukubwa au upana wa kikosi cha Simba , ninamaanisha ubora wa wachezaji wa timu hiyo.

Ni ukweli ulio wazi kwamba, kikosi cha sasa cha Simba kinaundwa na wachezaji wenye viwango vya juu na uzoefu mkubwa.

Hata hivyo, uwezo wa wachezaji wa timu hiyo kucheza dakika tisini kwa kasi ile ile pasipo kuchoka ni eneo jingine muhimu katika kufikia matarajio ya kikosi hicho.

Nani anayesababisha hali hii?

Kabla ya msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania  Bara, kikosi cha Simba kilikuwa kikijulikana kwa sifa ya kutomudu vyema mapambano ya dakika 90.

Simba haikuwa na uwezo wa kucheza vipindi vyote viwili kwa kasi ile ile. Iliweza kucheza kipindi cha kwanza kwa kasi lakini kadri  muda ulivyozidi kusonga kasi ilipungua.

Hata hivyo udhaifu huo  haukushuhudiwa msimu uliopita wa Ligi Kuu na hata katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Simba ilishiriki.

Wachezaji wa timu hiyo walionekana kuwa na nguvu dakika ya kwanza hadi ya tisini.

Hapa  ndipo tunapomkuta mtu anayeitwa Adel Zrane.

Raia huyu wa Tunisia ndiye mtaalamu wa mazoezi ya viungo katika kikosi cha Simba.

Zrane tangu alipoajiriwa na klabu hiyo, ameweza kuwafanya wachezaji kuwa ngangari kiasi cha kutosha.

Undani wake

Zrane anasema alizaliwa mwaka  1980 katika mji wa Sousse nchini Tunisia.

Anasema katika ukuaji wake alikuwa anapenda sana maisha ya soka.

Elimu yake

Zrane anamiliki leseni ya juu ya utaalamu wa viungo ‘Phisical fitnes’ambayo inatambulika na Shirikisho la Soka Ulaya ‘UEFA’ pamoja na shahada ya uzamivu ‘PHD’ ya maswala ya lishe na viungo.

MCHANGO UBINGWA SIMBA

Kocha huyo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuisadia Simba kupata ubingwa, kutokana na namna ambayo amewajenga wachezaji na kuwafanya kuwa imara.

“Mimi kazi yangu ni kuhakikisha wakati wote wachezaji wanakuwa imara ili kuwafanya waweze kumudu mifumo ya kocha Aussems,”anasema.

Zrane  amefanya kazi kubwa kwa kuwafanya  wachezaji kuwa tayari wakati wote na hata Aussems alipofanya mabadiliko haikuathiri kiwango cha uchezaji cha timu yake.

  ANAVYOITAZAMA SIMBA

Anasema anajisikia faraja kufanya kazi ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi na hasa baada ya kuhakikishiwa na mabosi wake kubaki nayo msimu ujao.

Anasema mafanikio ya kazi anayofanya na           kikosi cha Simba yanatokana na uelewano kati yake na wachezaji.

“Hakika wachezaji wamekuwa wasikivu kwa  kila kinachowafundisha au kuwaelimisha, hii inaifanya kazi yangu kuwa rahisi,”anasema.

Anasema endapo wachezaji wa Simba wataendelea kuwa na nidhamu ya hali ya juu, kama ilivyo sasa, basi watafika mbali zaidi.

Anasema,wapo baadhi ya wachezaji aliwakuta wakiwa wamekata tama ya kuendelea kucheza soka kutokana na kutokubalika kwa makocha waliopita  hatua  iliyowafanya kujaa viburi, lakini akapambana kuwanjenga kisaikolojia hadi wakabadilika.

“ Nafurahi sana kuwepo Simba, hasa katika nchi hii ya Tanzania, nafanya kazi yangu katika mazingira  mazuri na watu ambao wapo tayari, naweza kusema wachezaji  wote ni marafiki zangu, nawalea kwa kuwafanya wawe na nidhamu nzuri,”anasema Zrane.

Wachezaji wanamzungumziaje?

Pascal Wawa

Ni beki wa kati wa Simba. Raia huyu wa Ivory Coast, ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Asec Memos ya nchini humo anamsifu Zrane kwa kusema ni mtu anayeijua kazi yake sawa sawa.

Wawani miongoni mwa wachezaji wakigeni ambao wakati wanajiunga na timu hiyo hawakukubalika kwa mashabiki, hali hiyo ilitokana na uzito mkubwa walioonekana kuwa nao dimbani.

 “Ni zaidi ya kaka kwangu, amekuwa karibu na mimi na kunitia moyo  hasa nilipokata tamaa, pia alinijenga na kuanza kufanya vizuri mpaka leo hii nipo fiti kabisa,”anasema.

 HAROUNA NIYONZIMA

Niyonzima ni kiungo wa Simba, raia wa Rwanda, ambaye alisajiliwa akitoka Yanga.

Tayari amewachezea Wekundu hao kwa  misimu miwili.

Kiungo huyo ni minongoni mwa wachezaji  walioponea chupu chupu kufungashiwa virago msimu uliyopita kutokana na kushuka kiwango.

 Kuporomoka kwa kiwango kwa nahodha huyo wa zamani wa Rwanda kulisababisha asiaminiwe na hivyo kuwa mchezaji anayeanzia benchi.

Niyonzima amesema,  mpaka anafanikiwa kurejea katika ubora wake ni matokeo ya programu za kocha Zrane.

Anasema amemfanya kuwa na uwezo wa kucheza  dakika tisini kwa kiwango kile kile.

“Huwezi kuniambia kitu kwa huyu kocha, amenisaidia sana, kweli nilitaka niondoke kabisa Simba, lakini walishirikiana na kocha Aussems kunijenga kisaikolojia mpaka leo nipo sawa, nina imani kuwa bado nina misimu kadhaa mbele ya kucheza soka hapa,”anasema Niyonzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles