Imechapishwa: Tue, Dec 27th, 2016

ULANGA, KILOMBERO WAPITISHA MPANGO WA ARDHI

William Lukuvi

William Lukuvi

Na Ramadhan Libenanga-Kilombero

VIJIJI sita vilivyopo katika wilaya za Kilombero na Ulanga mkoani Morogoro vimepanga na kupitisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuwezesha umilikishaji ardhi katika vijiji vyote vya wilaya hizo.

Maamuzi hayo yamefanyika katika mikutano mikuu ya hadhara ya vijiji hivyo ambapo licha ya kupitisha mpango huo pia wamepitisha sheria ndogo ambazo zitawabana wale wote watakaokiuka sheria walizojiwekea ili kupunguza migogoro ya ardhi.

Akizungumza katika mikutano hiyo, Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Kilombero,  Siyabumi Mwaipopo alisema  katika kufanikisha kupitisha mpango huo walishirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wataalamu kutoka mpango wa kuwezesha umilikishaji ardhi (LTSP), sasa hatua hiyo itasaidia kulinda haki za wananchi katika umiliki wa ardhi.

Alisema LTSP walianza kuhamasisha wananchi hasa makundi maalumu hasa ya wanawake, vijana, wafugaji, watu wenye umelavu jambo ambalo litasaidia utekelezaji wa mpango huo wa matumizi bora ya ardhi.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

ULANGA, KILOMBERO WAPITISHA MPANGO WA ARDHI