24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ukuaji wa ajira rasmi na zisizo rasmi umeng’ang’ania kwenye asilimia 1.9

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

IMEELEZWA kuwa nafasi ya sekta ya mawasiliano kulipeleka taifa kwenye uchumi wa kati ina wastani wa asilimia nzuri kutokana na mchango mkubwa wa sekta za mawasiliano nchini.

Hayo yamo kwenye ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Benki ya dunia kupitia mtandao wake bonyeza hapa ‘https://data.worldbank.org/indicator/sl.uem.totl.zs?most_recent_value_desc=false‘, ambapo imeainisha kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 8 na soko la ajira rasmi na zisizo rasmi kubaki kwa asilimi 1.9.

Ripoti hiyo, imesema takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa Tanzania ina bahati kubwa kwa sababu kwa muongo mmoja uliopita tumekuwa na uchumi imara na ukuaji mkubwa wa pato la taifa kwa wastani wa asilimia hizo 8 ambao unachangiwa kwa kiasi fulani na ajira hizo.

Imesema mafanikio hayo makubwa ya ukuwaji wa kiuchumi, soko la ajira yamechangiwa kwa kiasi fulani na sekta binafsi, technolojia, ujenzi na mawasiliano na kuongeza kuwa maeneo hayo matatu na makampuni mbalimbali yametoa ajira kwa idadi kubwa ya watanzania.

Mtandao huo ulianisha kuwa kati ya sababu ambazo zinasaidia makampuni mengi katika sekta ya mawasiliano kufanikiwa katika suala la kutoa nafasi za ajira ni kuwa huduma zake zinahitajika katika sekta nyingine zote za uchumi.

Ilitoa mfano kuwa sekta ya mawasiliano ya simu, aina ya ajira ambazo sekta hii inatoa zinakwenda mbali ya namna ambavyo awali ilitazamwa, sekta hii ina mawakala wa fedha, wasambazaji na wauzaji wa huduma za simu, wataalamu wa huduma kwa wateja na wengineo.

Mtamdao huo uliendelea kueleza kuwa wigo wa soko la ajira unazidi kupanuliwa na sekta za mawasiliano kwani sekta hiyo pia inahitaji wataalamu toka maeneo mengine mengi, mfano wahandishi wa mitambo ya mawasiliano na wachambuzi wa takwimu.

Ulieleza kuwa Wapo wataalamu lukuki wa fani mbalimbali ambao wanahakikisha masaa 24 mitambo iko sawa kutuwezesha kupata huduma na kutumia simu zetu bila tatizo mfano kuperuzi mtandaoni, kununua bando, kutuma na kupokea pesa, SMS, na nyingine nyingi.

Mtandao huo uliitaja kampuni ya Tigo Tanzania ni mfano mmojawapo wa kampuni hizo kwani Kampuni hiyo inatajwa kama mwajiri muhimu nchini kwani ina zaidi ya wafanyakazi 115,000 wenye ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Mtandao huo pia uliishauri serikali kuwa haina budi kuendelea kuunga mkono sekta za mawasiliano na wadau wake ili kuendelea kusukuma zaidi gurudumu la maendeleo ya uchumi wetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles