27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ukawa yatoa tathmini ya ushindi wao

ReginaldMunisiNA MAULI MUYENJWA, DAR ES SALAAM

IKIWA zimebaki siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umetoa tathmini yake ya ushindi kwa asilimia 61 kwa wagombea wake wanaogombania nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

Tathmini hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Ukawa, Regnald Munisi, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uchaguzi huo.

Alisema tathmini hiyo waliifanya mikoa yote kwa sampuli ya watu 30,000.

“Tuna uhakika kwa ushindi wa asilimia 61, na kama ikishuka sana itakuwa asilimia 58, na ikipanda ni kwa asilimia 64, na mtaona itakavyokuwa katika matokeo, ndivyo itakuwa hivyo,” alisema Munisi.

Alisema hawataukubali mfumo wa kuhesabia kura kwa vifaa ambavyo hawana uhakika navyo, ikiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itagoma kuwashirikisha ili wajiridhishe navyo kabla ya kuvitumia kwa kudai kuwa wanawaingilia.

“Kila chama kinapaswa kuridhika na matumizi na utendaji wa mashine hizo za kuhesabia kura, hatutaweza kukubali kutumia mashine hizo kama zinaweza kuwa na matatizo,” alisema Munisi.

Aidha aliitaka NEC kutoa idadi ya mwisho ya vituo vya kupigia kura ili waweze kupeleka mawakala wao.

Alisema NEC imekuwa ikitoa idadi tofauti kwa vipindi tofauti kwa kuwa mwanzoni ilidai vituo vitakuwa 72,000, baadaye ikatangaza 65,000 na sasa 63,000.

“Wasiwasi ni kwamba NEC inaweza kutangaza idadi ya vituo vipya, na ikaongezeka wakati huu wa mwisho, hivyo inawezekana mawakala washindwe kuwepo katika vituo hivyo kama hatuvijui mapema,” alisema Munisi.

Pia aliitaka NEC kueleza kama kuna idadi ya watu iliyoongezeka katika daftari la wapigakura na ilikuwaje wasiwepo awali.

“Watueleze tujue ni wangapi na kuona kama itawezekana kwa kuwa kama ni wengi kama milioni moja, hatuwezi kukubali kwa kuwa hatuna uhakika nao, lakini kama ni wachache kama 100 tunaweza kuelewana baada ya kuongea,” alisema Munisi.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles