30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UJUE UGONJWA WA HIMOFILIA

Na Aziza Masoud,

HIMOFILIA ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wa kuganda ambao unasababishwa  ukosefu wa kiwango cha kutosha cha chembechembe za protini zinazotakiwa kugandisha damu na  kusababisha damu kuvuja kwa muda mrefu.

Ugonjwa  huu ambao  asilimia 30  ya wagonjwa huzaliwa nao kutokana na mabadiliko ya vinasaba pia hurithiwa na huwakumba jinsia zote.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Stella Rwezaura anaeleza kuwa  asilimia 97 ya wagonjwa wa himofilia hawajui kama wanaougonjwa huo na hawajawahi kupatiwa vipimo vyovyote ili kujua hali ya ugonjwa.

Anasema mtu mwenye ugonjwa huu ataishi nao kwa maisha yake yote bila kupona lakini una uwezo wa kutibika.

Aina za Himofilia

Anasema kuna aina mbili za  himofilia ikiwemo wagonjwa wengi kupata himofilia A,mara nyingi wagonjwa wa kundi hili hawana chembechembe za kugandisha damu  .

Anabainisha kundi lingine ni Hemofilia B,mara nyingi huwapata wagonjwa wachache wenye upungufu wa chembechembe  namba 9.

“Kwa pamoja makundi hayo yote mawili ya Hemofilia A na B wote kwa pamoja huvuja damu kwa muda mrefu kuliko wagonjwa wa kawaida,”anasema Dk.Stella.

Anasema mgonjwa wa himofilia kwakuwa anakuwa anavuja damu katika viungo  inamfanya anakosa nguvu na kushindwa kufanya shughuli zake za kila siku.

Dalili za himofilia

Anabainisha dalili za Ugonjwa huo  zinazoonekana kwa macho ni pamoja na kutokwa damu mfululizo kwa muda mrefu unapotokea mchubuko, kukatwa au kujikata, kutoneshwa ama jitonesha kidonda .

Itaendelea wiki ijayo
 Makala haya yameandaliwa  kwa msaada wa Chama Cha Madaktari wa Himofilia Tanzania .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles