27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ujerumani yaongeza miaka minne misaada ya jeshi

Mwandishi wetu

SERIKALI ya Ujerumani kupitia Mpango wa Kusaidia Majeshi Rafiki, imekubali kuongeza kipindi cha kutoa misaada kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa miaka minne zaidi kuanzia mwaka 2021 hadi 2024.

Katika hatua hiyo, pamoja na mambo mengine, kupitia mpango huo, itajenga hospitali ya  eshi yenye kiwango cha “Level 4” mkoani Dodoma.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Wäechter, akiwa na ujumbe kutoka Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, alitangaza uamuzi huo jana Ikulu  Dar es Salaam alipokutana na   Rais John Magufuli.

Ilisema Dk. Wäechter alisema katika ushirikiano huo, Ujerumani kupitia Timu ya Ushauri ya Wataalamu wa Kijeshi (GAFTAG) Ujerumani itaongeza mafunzo na vifaa vya ulinzi wa amani, itaendelea kufundisha madaktari wa jeshi na kutoa vifaa vya matibabu na kutoa mafunzo ya ulinzi wa amani.

“Katika ushirikiano wa sasa utakaoishia 2021, kati ya Juni 2017 na Machi 2019, Ujerumani imejenga Hospitali ya Kanda huko Monduli mkoani Arusha ambayo imewekewa vifaa tiba vinavyotumia teknolojia ya kisasa na itakayotumiwa kama hospitali ya rufaa ikisaidiana na Hospitali ya Jeshi ya Lugalo   Dar es Salaam.

“Ujenzi wa hospitali hiyo uligharimu Sh bilioni 5.947 ambako Sh milioni 346.8 kati yake zimetolewa na Serikali ya Tanzania,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema ufadhili mwingine uliotolewa ni upanuzi na uboreshaji wa Chuo cha Sayansi na Tiba cha Lugalo, ujenzi wa karakana za jeshi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Shinyanga na Mwanza.

Nyingine ni  ujenzi wa idara ya dharura ya Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Hospitali ya Kanda iliyopo Bububu – Zanzibar, uboreshaji wa hospitali za kanda zilizopo Zanzibar, Mbeya, Mwanza na Tabora, msaada wa magari na vifaa tiba.

Ilisema, Rais Magufuli ameishukuru Ujerumani kwa kuendeleza na kuukuza uhusiano na ushirikiano na Tanzania na amemhakikishia Balozi Wäechter kuwa Serikali ya Tanzania itahakikisha misaada yote inayotolewa inaleta manufaa yaliyokusudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles