UJERUMANI YAKABIDHI MIILI YA WALIOUAWA NAMIBIA

0
645

 

BERLIN, UJERUMANI


Serikali ya Ujerumani jana ilikabidhi mabaki ya raia wahafidhina wa Namibia, ambao waliuawa katika mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa wakati wa utawala wa kikoloni wa Ujerumani.

Miili hiyo ilikabidhiwa kwa ujumbe kutoka taifa hili la kusini mwa Afrika, ambalo lilikuwa koloni ya Ujerumani kati ya mwaka 1884 na 1915.

Maelfu ya watu waliuawa wakati wa mfululizo wa maandamano yaliyofanyika kupinga utawala dhalimu wa wakoloni kati ya mwaka 1904 na 1908.

Wengine walikufa kutokana na njaa na wengine kutokana na madhila ya kufungwa na kuteswa katika kambi za mateso.

Wanahistoria wanakadiria kuwa watu 65,000 wa kabila la Herero na 10,000 wa jamii ya Nama waliuawa.

Idadi hii iliwakilisha takribani asilimia 80 na 50 ya idadi ya jumla ya makundi hayo kipindi hicho.

Ujerumani haijawahi kuomba radhi rasmi baada ya kutokea mauaji hayo au kutoa malipo ya moja kwa moja.

Watu wa jamii hizo mbili waliwasilisha kesi katika Mahakama ya Marekani ambako walidai fidia.

Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje Ujerumani, Michelle Muentefering, aliongozana na mabaki hadi mji mkuu wa Namibia, ambapo mazungumzo zaidi yamepangwa kesho.

Jana ilikuwa mara ya tatu ya mabaki ya binadamu kupelekwa nchini Namibia.

Mabaki hayo yalipelekwa Ujerumani kwa mara ya kwanza kufanyiwa utafiti, ambao ulitangulia ule wa Wayahudi walioangamizwa wakati wa utawala wa Nazi, Ujerumani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here