24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Uingereza yadai Iran ilijaribu kuizuia njia meli yake

LONDON -UINGEREZA

UINGEREZA imedai meli za kijeshi za Iran zilijaribu kuizuia njia meli ya mafuta inayomilikiwa na Uingereza lakini zikaondoshwa na meli yake ya kivita, madai ambayo Iran imeyakanusha vikali.

Taarifa hizi mpya zimekuja ikiwa ni wiki iliyopita tu tangu nchi hizo mbili ziingie kwenye vita ya maneno baada ya Uingereza kudaiwa kuizuia meli ya mafuta ya Iran kwenye eneo la Gibraltar na hivyo Iran kutishia kufanya tukio kama hilo.

Kwa mujibu wa Uingereza, tukio hilo lilitokea juzi Jumatano kwenye mlango bahari wa Hormuz, muda mchache baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kurejea vitisho vyake vya kuongeza vikwazo vikali dhidi ya Iran.

Awali, kituo cha televisheni cha Marekani, CNN, kiliripoti kuwa boti za Iran zilijaribu kuiteka meli hiyo ya mafuta ya Uingereza, lakini zikafukuzwa na meli ya kijeshi ya Uingereza.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza alisema kuwa mashua tatu za Iran zilijaribu kuizuia njia meli hiyo iitwayo British Heritage inayomilikiwa na kampuni ya mafuta ya Uingereza, BP.

“Kinyume na sheria za kimataifa, mashua tatu za Iran zilijaribu kuizuia njia meli ya kibiashara, British Heritage, kwenye mlango wa bahari wa Hormuz.

“Meli ya kijeshi ya HMS Montrose ililazimika kujiweka baina ya mashua hizo za Iran na British Heritage na kutoa onyo la mdomo kisha mashua hizo  ziliondoka.” Ilieleza taarifa hiyo ambayo pia ilitoa wito kwa Iran kujiepusha na kuichafua hali ya usalama kwenye eneo hilo.

Hata hivyo, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran – chombo chenye nguvu kubwa ya kijeshi ambacho Marekani inakilaumu kwa kufanya mashambulizi kadhaa dhidi ya meli za mafuta tangu mwezi Mei, kilikanusha vikali tuhuma za kujaribu kuiteka au kuizuia njia meli hiyo ya mafuta ya Uingereza.

“Hakujatokea makabiliano yoyote ndani ya saa 24 zilizopita kati yetu na meli yoyote ya kigeni, zikiwemo za Uingereza.” Ilisema taarifa fupi iliyotolewa na kikosi hicho.

Taarifa hizi zinachochea zaidi uhasama unaoendelea kwenye eneo hilo la ghuba, ambalo tayari liko kwenye hatihati kutokana na mkwamo baina ya utawala wa Rais Trump wa Marekani na Iran juu ya mpango wa nyuklia wa taifa hilo la Kiislamu.

Juzi Rais Hassan Rouhani wa Iran aliionya Uingereza kwamba itakumbwa na matokeo mabaya ambayo hakuyataja, kutokana na hatua ya nchi hiyo kuikamata meli ya mafuta ya Iran kwenye eneo la Gibraltar.

Maafisa kwenye eneo hilo, ambalo linamilikiwa na Uingereza licha ya kuwa kwake Uhispania, walidai kuwa meli hiyo ilikuwa ikielekea Syria, ambayo imewekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya, huku Marekani nayo ikiwa na vikwazo vyake dhidi ya mafuta ya Iran.

Iran ilikilaani kitendo hicho ilichokiita kuwa ni cha kiharamia, huku Uingereza ikikanusha madai ya maafisa ya Gibraltar kuwa imeishikilia meli hiyo kwa maagizo ya Marekani.

Mkuu wa majeshi ya Ufaransa Francois Lecointre, jana alisema baada ya Uingereza kuishutumu Iran kuzisumbua meli za mafuta za nchi hiyo hali ya wasi wasi katika eneo la Ghuba haielekei kufikia kiwango cha kutoweza kudhibitiwa.

Lecointre alisema hata hivyo kuna hali ya kupimana nguvu kati ya Marekani na Iran, ambayo inaweza wakati wowote kufikia hatua ya kutoweza kudhibitika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles