27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uingereza yaanza kufanyia majaribio dawa mpya

LONDON, UINGEREZA

DAWA mpya iliotengenezwa na wanasayansi wa Uingereza kutibu ugonjwa wa Covid 19 inafanyiwa majaribio katika Chuo Kikuu cha Southampton.

Ikiwa imetenegenezwa na kampuni ya Synairgen, inatumia protini kwa jina Infterferon Beta, ambayo hutoka katika mwili wa binadamu anapopata maambukizi ya virusi.

Matokeo ya majaribio hayo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Juni.

Kwa sasa kuna dawa chache zinazoweza kutibu virusi hivyo huku madaktari wakitegemea kinga ya wagonjwa wao.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Synairgen iliyo na makao yake mjini Southampton, Richard Marsd alisema jana kuwa Interferon Beta ni dawa inayolinda mwili wa binadamu dhidi ya virusi, ikionya dhidi ya shambulio la virusi.

Alisema virusi vya corona hujaribu kukabiliana na uzalishaji wake kama mpango wa kutaka kukwepa mfumo wa kinga mwilini.

Dawa hiyo ina muundo maalum wa interferon beta inayowekwa moja kwa moja kwenye njia za hewa wakati zilizopo na virusi, kwa matumaini kwamba kipimo cha protini moja kwa moja kitatoa majibu ya kupambana na virusi hata miongoni mwa wagonjwa ambao kinga zao tayari ni dhaifu.

Interferon Beta hutumika sana kutibu ugonjwa wa kupooza. Synairgen tayari imethibitisha kwamba maandalizi yake yanaweza kuimarisha kinga katika mapafu ya mgonjwa mwenye asthma na magonjwa sugu ya mapafu.

Lakini tunaweza kujua iwapo inaweza kukabiliana na Covid-19 baada ya kufanyiwa majaribio kadhaa miongoni mwa binadamu.

Kaye Flitney (67) ni miongoni mwa wagonjwa waliojumuishwa katika majaribio hayo yaliorekodiwa na BBC panorama .

Inahitaji wagonjwa wa Covid-19 kama yeye, kuvuta dawa hiyo kwa kutumia nebulizer ili kuuingiza katika mapafu.

Kaye anapata shida kuketi katika kitanda chake cha hospitali na anakohoa anapoweka dispenser katika mdomo wake.

Alisema kwamba mara ya kwanza alipogundua ana virusi vya corona fikra yake ya kwanza haikuwa sio kuangalia afya yake.

”Nilitishika kwa sababu mume wangu ana tatizo la moyo. Itamuua”.

Alisema kwamba utumizi wa dawa hiyo haujamsababishia tatizo lolote. “Huwezi kujua kwamba unaitumia hadi pale utakapomaliza. Sio mbaya. Naweza kuitumia nyumbani”.

Watu 75 waliojitolea kufikia sasa walitoka katika hospitali 10 nchini Uingereza .

Nusu yao watapatiwa dawa hiyo huku wengine waliosalia wakipatiwa dawa kama hiyo lakini ya bandia.

Hakuna anayehusishwa katika majaribio hayo anajua ni wagonjwa gani waliopatiwa dawa ya aina gani hadi pale vipimo hivyo vitakapokamilika.

“Iwapo utajua kwamba ni dawa unaweza kuwa na upendeleo,” anaelezea sandy Aitken, muuguzi anayetoa dawa hiyo.

Matumaini ni kwamba, itaonyesha kwamba wagonjwa wanaopatiwa dawa hiyo wanaimarika ikilinganishwa na wale ambao hawakupatiwa, kulingana na Profesa Tom Wilkinson wa Chuo Kikuu cha Southampton.

Majaribio ya dawa ya kampuni ya Synairgen ni mojawapo ya vipimo vya haraka vilivyoanzishwa na Serikali.

Mpango huo kwa jina Accord kama unavyojulikana unalenga kutengeneza dawa mpya ya wagonjwa wa corona. Awamu ya kwanza itashirikisha dawa nyengine sita.

Zaidi ya tiba 100 kote duniani zinafanyiwa majaribio na dawa kwa jina remdesivir ambayo ilitengenezwa kutibu ebola imeonyesha matumaini.

Maofisa wa Marekani wamedai kwamba kuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba inaweza kuwaponya watu walio na virusi vya corona.

Matokeo ya awali ya Interferon Beta yanatarajiwa mwisho wa mwezi Juni.

Hatua hiyo huenda ikachukua miezi kadhaa, ijapokuwa Serikali itafanya kazi haraka iwezekanavyo.

Iwapo itaonekana inafanya kazi, dawa hiyo pamoja na kifaa kinachotumika kuivuta mapafuni italazimika kutengenezwa kwa wingi. BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles