24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

UHAMIAJI KILIMANJARO WATAKIWA KUZINGATIA HAKI UTOAJI PASPOTI

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Watumishi wa Idara ya Uhamiaji wanaohusika na utoaji wa huduma ya hati ya kusafiria (passport) mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kutoa huduma kwa haki bila ubaguzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira leo Mei 30, katika uzinduzi wa huduma ya pasipoti kwa njia ya kielektroniki mkoani hapa.

“Aidha kwa kuwa huduma hii ni ya kisasa zaidi naamini wananchi watahudumiwa vizuri bila usumbufu wowote na hii pia itasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi.

“Lengo la kuanzishwa kwa pasipoti mpya ya kielektroniki ya Afrika mashariki Tanzania ni kukidhi matakwa ya usalama wa nchi na kukidhi viwango vilivyopendekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia usafiri wa anga lakini pia zinatoa fursa ya utambulisho wa pamoja wa raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanapokuwa nchi za nje,” amesema Mghwira.

Kwa upande wake Kamishna wa pasipoti na uraia, Gerald Kihinga, alisema kuwa tangu kuanza kwa huduma hiyo ya utoaji pasipoti kwa njia ya kielektroniki Januari 31, mwaka huu jumla ya  pasipoti 15,700 zimetolewa.

“Katika Pasipoti hizo, 46 zimetolewa kwa watumishi (Pasipoti ya Utumishi) Pasipoti za kidiplomasia  237 na Pasipoti Maalumu za kidiplomasia tano,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles