24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UFARANSA KUTOA BILIONI 150/- UJENZI UWANJA WA NDEGE DAR

Na JUSTIN DAMIAN,

SHIRIKA la Maendeleo la Ufaransa (AFD), lipo katika majadiliano yatakayoiwezesha Serikali kupata mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 65 (zaidi ya Sh bilioni 150) kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Mwakilishi wa shirika hilo hapa nchini, Emmanuel Baudran, aliliambia MTANZANIA katika kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa linaloendelea jijini Dar es Salaam, kuwa mkopo huo unalenga kuboresha uwanja huo – terminal 2, ili uweze kuendana na ongezeko la abiria.

Baudran alisema majadiliano hayo yapo katika hatua nzuri na kuongeza kuwa mkataba wa mkopo huo unaweza kusainiwa mwezi ujao.

“Tunaamini kuwa usafiri wa anga ni kichocheo muhimu cha maendeleo na Tanzania imekuwa ikipokea watalii wengi. Biashara kati ya mkoa mmoja na mwingine zinakua pia na kwa kuwa nia yetu ni kusaidia sekta zenye mchango kwa maendeleo, tunaona eneo hili ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,” alisema Baudran.

Alisema shirika hilo lipo katika majadiliano na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo wa masharti nafuu kukarabati viwanja vingine vya ndege vilivyopo katika mikoa mbalimbali.

“Tanzania ina  viwanja vya ndege zaidi ya 15, ikiwa ni pamoja na vikubwa na vidogo. Baadhi ya viwanja hivi havipo katika hali nzuri na AFD ipo tayari kusaidia ukarabati wake,” alisema.

Alisema katika mpango wa ukarabati wa viwanja 11 vya ndege ambao Serikali inao, shirika hilo lipo tayari kufadhili baadhi ya viwanja ambavyo Serikali itatoa kipaumbele na kutaka fedha kwa ukarabati na upanuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles