28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Uelewa kuhusu Mahakama ya Afrika utaleta hamasa nchi za AU

ELIYA MBONEA-ARUSHA

Uelewa wa wadau kuhusu uwapo wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), utaleta hamasa kwa nchi zaidi za Umoja wa Afrika (AU) kuridhia Itifaki iliyoanzisha Mahakama hiyo kupokea kesi za za watu binafsi na mashirika yaisyo ya Kiserikali (NGO’s).

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 22,na Rais wa Mahakama ya Afrika Jaji Sylvain Ore’ yenye Makao Makuu mjini Arusha, akiwa nchini Djibouti kwenye mazungumzo na wadau mbalimbali kwa lengo la kuitangaza Mahakama hiyo ya Umoja wa Afrika (AU).

“Ili Mahakama ifanikishe malengo yake na pia kuimarisha mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika,nchi nyingi za Umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa mujibu wa kifungu cha 34(6),”alisema Jaji Ore.

Amesema ziara hiyo iliyoanza Mei 21 hadi Mei 24, mwaka huu wanatarajiwa kukutana na Waziri  Mkuu wa Djibouti, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Sheria na Spika wa Bunge ambapo watakuwa na semima inayolenga kukuza uelewa wa wadau hao juu ya uwepo wa Mahakama na jinsi inavyoendesha shughuli zake ikiwamo kupokea mashauri.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliendelea kueleza tangu mwaka 2010, AfCHPR imefanikiwa kuendesha programu mbalimbali zinazolenga kutoa elimu ya uwepo na shughuli zake katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwamo Chad, Ethiopia, Afrika ya Kusini, Ghana, Malawi, Kenya, Uganda, Zambia, Morroco na Tunisia.

Nchi nyingine zilizotajwa ni pamoja na Ivory Coast,Cape Verde,Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi,Misri na GuineaBissau.

Mahakama hiyo ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ilianzishwa mwaka 2006 na kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2008.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles