Imechapishwa: Thu, Jul 12th, 2018

UDP TANGA YAANZA MCHAKATO WA UTEUZI WA WAGOMBEA UDIWANI

Na Oscar Assenga

Chama cha UDP mkoani Tanga kimeanza mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani kwa kata za Makorora na Mabokweni jijini Tanga.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Tanga, Mhina Peter Mhina amesema wameanza mchakato baada ya kumalizika kikao cha kamati kuu kilichoketi Makao Makuu ya chama hicho chini ya Mwenyekiti wa Taifa John Cheyo.

Amesema kwa upande wa Kata ya Makorora wamempitisha Ibrahim Nyakunga huku Kata ya Mabokweni mchakato wa kumpata mgombea ukiendelea.

Hata hivyo alisema pia watasimamisha wagombea kwenye ngazi ya Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini wakati  mchakato huo utapotangazwa.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

UDP TANGA YAANZA MCHAKATO WA UTEUZI WA WAGOMBEA UDIWANI