24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Uchumi Tanzania kupea mwaka 2026

CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

UTAFITI unaonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi kufikia mwaka 2026.

Kwa mujibu wa utafiti wa Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo cha Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani kinakadiria uchumi wa Tanzania utakua kwa asilimia 6.15 katika kipindi hicho.

Utafiti huo unaipaisha Tanzania kufikia ya nne kwa uchumi wake kukua kwa kasi wakati huo.
Kwa sasa India ndiyo inayoongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi ya 7.89 ikifuatiwa na Uganda 7.46 na Misri ya tatu (6.63).


Utafiti huo ulikadiria ukuaji kwa kutumia mchangamano wa kiuchumi, kipimo kimoja ambacho huangazia uchangamano wa uzalishaji na uchangamano wa uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za kuuzwa nje katika taifa jingine.

Katika Ripoti hiyo ya Harvard ilieleza kwamba kampuni ambazo zimefanya mabadiliko chanya na kuingiza uchangamano katika sekta mbalimbali za uchumi kwa mfano India na Vietnam ndizo zitakazokua kwa kasi zaidi katika mwongo mmoja ujao.

Baada ya mwongo mmoja wa ukuaji wa kiuchumi ambao uliongozwa na mafuta na bei za bidhaa, wamebaini kwamba mambo yamebadilika na sasa mataifa yenye uchumi unaotegemea sekta mbalimbali ndiyo yatakayofanya vizuri zaidi.


Baada ya Uganda na Tanzania, Kenya ni ya kumi katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kukua kwa kasi zaidi mwaka 2026 ambapo ukuaji wake utakuwa kwa asilimia 5.87.


Mataifa hayo ya Afrika Mashariki yameshuhudia wafanyakazi wake wengi wakiacha kilimo na kuingia kwenye shughuli za viwanda.


Zipo taasisi ambazo zimekuwa zikifanya jitihada ya kufanya tafiti ambazo zitasaidia ukuaji uchumi wa nchi kwa kuangalia rasilimali zilizopo na mazingira halisi ya nchi.


Miongoni mwa taasisi hiyo ni pamoja na Taasisi ya uchambuzi mambo ya Sera na Uchumi (REPOA), ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuchagiza uchumi wan chi katika Nyanja mbalimbali.


Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA . Dk.Donald Mmari anasema ipo haja kwa wachambuzi kuangalia kwa makini viashiria zaidi ya kimoja vinavyochochea ukuaji uchumi hapa nchini.


Anasema ni vyema kuangalia uchumi wa ndani kwa kuanzia ngazi ya chini ili kushirikisha vyanzo mbalimbali vinavyochangia ukuaji uchumi.


“Kila mmoja akiwa mshiriki katika ukuaji uchumi kwa kuibua fursa na kuzitambua kila eneo lina uwezo wa kuchochea uchumi kukua na tafiti nyingi zimebaini hili,”anasema Mmari.


Anasema ni bora kuangalia namna bora ya kuangalia fursa katika ukuaji uchumi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.


Mmari anasema REPOA itahakikisha matokeo ya tafiti zao zinawafikia wananchi wote ili kuondoa changamoto zilizopo ndani ya jamii hasa wale wenye kipato cha chini.


“Mfumo wa serikali kwa upande wa halmashauri sio rahisi kufanya katika shughuli za kiuchumi kutambua fursa, kujenga uwezo wenye tija zaidi,”anasema Mmari.


Naye, Mkurugenzi wa Tafiti za Kimkakati, Dk.Jamal Msami anasema, ukizungumzia maendeleo ni vyema kuangalia mifumo inayotumika katika halmashauri zote nchini ili kubaini jambo hilo.
Anasema ipo haja ya upatikanaji na uendelezaji fursa ili zilete matokeo ndani ya jamii.


‘Hapa nchini kuna halmashauri 185 na kwa Tanzania Bara na Visiwani kuna mikoa 31 hivyo ni vyema kufungua fursa zilizopo ili kuondoa mkwamo na kufikia maendeleo,’anasema Msami.


Msami anaongeza kuwa wanahabari waisaidie jamii kujikwamua ambapo ukizungumzia jambo lenye sura ya kijamii kweli lifanane.
Anasema tofauti ya kimazingira isiwe changamoto bali ni fursa ya kufikia maendeleo.


Naye, Mkuu wa Utafiti REPOA, Dk.Blandina Kilama anasema REPOA imelenga kuangalia kila nafasi ina wajibu gani katika kukuza uchumi wa nchi kwa maendeleo ya uchumi wa ndani.
Blandina anasema ni vyema kukawa na ushirikishwaji na upatikanaji wa fursa kuanzia ngazi ya chini.


“Ushirikishwaji na upatikanaji wa fursa kuanzia ngazi ya chini kutasaidia kukuza uchumi kwa kasi zaidi,” anasema Dk.Blandina.
Anasema wanaendelea kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitasaidia jamii kujikwamua kimaisha na kiuchumi.


Anaongeza kuwa mkutano wanaotarajia kufanyika wiki hii ana imani utatoa fursa kubwa kwa wachambuzi na watafiti kupata fursa zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles