UCHAGUZI MDOGO WA VIONGOZI BODI YA LIGI KUFANYIKA NOVEMBA 17

0
745

Bethsheba Wambura, Dar es SalaamUchaguzi mdogo wa kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kujaza nafasi zilizo wazi utafanyika Jumamosi Novemba 17,2018 jijini Dar es Salaam.

Fomu kwaajili ya Wagombea zitaanza kutolewa Septemba 21,2018 kwenye Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea ni saa 10 kamili jioni Septemba 25,2018.

Taarifa iliyotolewa leo  na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF Cliford Ndimbo imesema nafasi zitakazowaniwa ni mwenyekiti, mjumbe mmoja wa kuwakilisha Klabu za Ligi Kuu (PL), mjumbe mmoja kuwakilisha Klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL),na mjumbe mmoja wa kuwakilisha Klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL).

Amesema ada ya fomu kwa nafasi za Mwenyekiti ni sh.200,000 wakati nafasi nyingine zilizobaki ni sh.100,000.

“Uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za TFF toleo la 2013 na wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ni marais au wenyeviti wa Klabu husika, hivyo wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au marais wa Klabu husika,”amesema.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here