25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UBER KUFUNGUA VITUO VYA HUDUMA

Kampuni inayotoa huduma ya usafiri wa Taxi jijini Dar es Salaam, Uber Tanzania iko kwenye mchakato wa kufungua vituo kwa ajili ya kuhudumia wateja wasiokuwa na ‘smartphone’.

Mkurugenzi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo amesema vituo hivyo ni maalumu kwa wateja ambao hawana smartphone au ambao simu zao zimeisha chaji na kuzimika au ambao hawajui namna ya kutumia huduma hiyo kwenye simu ambapo watasaidiwa na wahudumu watakaokuwapo eneo hilo kuomba huduma ya usafiri bila malipo.

“Uber ni huduma ya usafiri wa kuaminika, bei nafuu na salama na katika kuwajali wateja wetu ambao wakati mwingine wanakuwa wameishiwa chaji kwenye simu au hawana smartphone na wanahitaji huduma lakini wanashindwa kutokana na sababu hizo au nyingine,” amesema Msemo.

Pamoja na mambo mengine, Msemo amesema kupitia huduma ya Uber wamefanikiwa kutengeneza ajira zaidi ya 1,000 kupitia madereva waliojisajili na Uber tangu kuanzishwa kwake nchini Juni, mwaka jana.

“Pamoja na mafanikio hayo ziko changamoto zinazotukabili ikiwamo zikiwamo kuhitajika zaidi mikoani ambako tunatarajia kuanza kusambaza huduma hiyo ili kuwaridhisha wateja wetu,” amesema.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Uber, Janeth Kimboi amesema kampuni hiyo inatoa huduma katika nchi 80 duniani ambapo kwa Afrika nchi inayoongoza ni Afrika Kusini ambapo Uber ilianzishwa mwaka 2013, Nairobi mwaka juzi na Dar es Salaam, mwaka jana.

Uber ni huduma ya usafiri inayotolewa kupitia programu iliyounganishwa kwenye simu ili kumuwezesha mteja kufanya mawasiliano na dereva aliye karibu na eneo alilopo mteja kupitia ramani maalumu ya google baada ya kuomba huduma hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles