33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ubalozi wa Marekani wampongeza bosi Jamii Forums

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

UBALOZI wa Marekani nchini Tanzania, umempongeza Mkurugenzi wa mitandai ya Kijamii ya Jamii Forums,  Maxence Melo, kwa kutangazwa mmoja wa washindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa mwaka 2019, tuzo inayotolewa na Kamati ya Ulinzi kwa Waandishi wa Habari.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Ubalozi wa Marekabi hapa nchini, ilieleza kwamba pamoja na kukabiliwa na changamoto nyingi za kisheria, Maxence Melo na Jamii Forums wameendelea kuwa mstari wa mbele katika kutetea uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari nchini.

“Tanzania inajivunia historia kubwa iliyosheheni mchango mkubwa wa vyombo vya habari, kuanzia mchango wa Radio Tanzania Dar es Salaam katika ukombozi wa Afrika, kuimarisha umoja wa Afrika na kukuza amani na haki.

Kutambuliwa kwa Maxence Melo  na kutunukiwa kwake tuzo hii kunatukumbusha urithi huu muhimu wa historia ya nchi hii; urithi ambao unatishiwa pale ambapo matukio ya  ukiukwaji wa haki, unyanyasaji na hata watu kupotea zinapogubika utamaduni wa maendeleo ya kijamii yanayosukumwa na vyombo vya habari.
“Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania unatoa wito kwa Serikali ya Tanzania kulinda urithi huu wa kihistoria kwa kuimarisha usalama wa waandishi wa habari na kutokomeza hali ya wale wanaowadhuru kutokuchukuliwa hatua zinazostahili,” ilieleza taarifa hiyo ya ubalozi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles