33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UBAKAJI WAONGEZEKA PWANI

ubakaji

NA GUSTAPHU HAULE, PWANI

WIMBI la makosa ya ubakaji limezidi kuongezeka mkoani Pwani, kutoka 257 kwa takwimu za Januari hadi Septemba 2015 hadi kufikia 310 kwa Septemba 2016.

Tofauti hiyo ni ya makosa 53, sawa na asilimia  21, ambapo makosa ya kulawiti mwaka 2015 yalikuwa 42, wakati mwaka 2016 yalikuwa 36, ikiwa ni tofauti ya makosa 6, sawa na asilimia 14, huku mimba zikipungua kutoka 36 hadi 29.

Takwimu hizo zilitolewa juzi na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Boniventura Mushongi, katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika mjini Kibaha na kuwashirikisha madereva wa bodaboda.

Mushongi alisema utafiti uliofanywa na Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia na Watoto umebaini kuwa, makosa hayo yanasababishwa na hali ngumu ya maisha pamoja na uzembe wa wazazi wanaoshindwa kuwakemea watoto wao.

Aidha, aliwaomba wazazi kuhakikisha wanasimamia malezi ya watoto wao kwa karibu, kwani kuwaacha peke yao huchangia mmomonyoko wa maadili unaosababisha watoto kuingia kwenye matendo maovu.

Mushongi alisema takwimu zinaonyesha kuwa, kila watuhumiwa 10 waliokamatwa na makosa mbalimbali ya ukatili wa kijinsia watu watatu ni madereva wa bodaboda, hivyo aliwaomba kujiepusha na matendo hayo na badala yake waangalie kwanza maisha yao.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles