27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ubakaji bado tatizo kwa watoto

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa takwimu za ukatili wa kijinsia kwa watoto huku akitaja ubakaji kuongoza kutokana na kuongezeka kila mwaka.

Waziri Ummy ametoa majibu hayo kwa njia ya maandishi akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Ruge (Chadema), aliyetaka kujua mkakati wa serikali kudhibiti ubakaji.

“Kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani ulawiti na ubakaji kwa wanafunzi vinavyofanywa baina ya wanafunzi wenyewe kwa wenyewe au watu wa karibu katika familia, je, serikali ina mkakati gani wa dharura kudhibiti matendo hayo?,” ameohoji.

Akijibu swali hilo Ummy amesema tatizo la ukatili wa kijinsia kwa watoto bado ni kubwa ambapo Takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambapo mwaka 2017 matukio yalikuwa 13,457, mwaka 2018 matukio 14,419 na mwaka 2019 matukio 15,680.

“Aidha, kwa mwaka 2019 vitendo vya ukatili vilivyoongoza ni Ubakaji (6,506), mimba za wanafunzi (2,830) na Ulawiti (1,405).

“Mikakati ya serikali katika kukabiliana na ulawiti pamoja na ubakaji ni kutoa elimu kwa jamii kupitia watu mashuhuri, viongozi wa kisiasa, dini na mila ili kushiriki katika kubadilisha tabia na mienendo ya baadhi ya watu wanaoendeleza tabia za aina hiyo katika jamii kwa kuchukua hatua kali za kisheria kuwafikisha mahakamani wale wote wanaotenda makosa hayo ili haki itendeke kwa mujibu wa Sheria.

“Pia kuna huduma za simu bila malipo kwa watoto ambayo inawezesha jamii kutoa taarifa za vitendo vya ukatili,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles