27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UBA,CRDB kusapoti umeme maporomoko ya Rufiji

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

BENKI ya UBA Tanzania na Benki ya CRDB, zimefikia makubaliano ya kushiriki kuunga mkono ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji Hydro electric Power Project (RHPP) kwa kutoa Dola za Kimarekani milioni 737.5 ambazo ni sawa na Sh Trilioni 1.7.

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa benki ya UBA, Usman Isiaka amesema fedha hizo ni dhamana ya benki inayotakiwa na mkandarasi katika mradi huo ambao utagharimu Sh trilioni 6.6.

“Kwa mujibu wa masharti ya mkataba huo, umoja huo unahitajika kutoa dhamana za benki za kigeni na za ndani zikiwa ni jumla ya Dola za Kimarekani milioni 737.5 kupitia utekelezaji wa mradi na dhamana ya malipo ya awali kwa mradi huo.

“Kwa kuanzia, Benki ya CRDB na UBA zimeshirikiana na Benki ya Afrika Export-Import (Afrieximbank) na benki nyingine za Misri kutoa dhamana za benki kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambapo sehemu ya dhamana hizo tumezitoa hapa leo (jana),”alisema Isiaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya UBA, Balozi Tuvako Manongi amesema miradi yote mikubwa ya uchumi ambayo serikali ya awamu ya tano inafanya haiwezi kukamilika bila bei ya umeme kushuka.

“Ndio maana sisi tukajumuika kuunga mkono mradi huu wa umeme ambao unagharimu fedha nyingi, hivyo tuna imani baada ya mradi huu kukamilika bei za umeme zitashuka,”alisema Balozi Manongi.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema wameamua kuunga mkono kwa kushirikiana na serikali katika mradi huo na kwamba uwezo na nia wanao.

“Tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio haya kwa kutoa fedha hizi na tutaendelea kushirikiana na serikali, lakini pia lazima tuishukuru Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuweka mazingira mazuri ya mabenki,”alisema Nsekela.

Mkurugenzi wa Tanesco, Tito Mwinuka amesema mradi huo utatekelezwa kama walivyokubaliana na kwamba pamoja na gharama yake kuwa kubwa lakini faida yake ni kubwa.

Kwa upande wake, Naibu Gavana wa BoT, Dk. Bernard Kibese amesema bila umeme wa bei rahisi nchi haiwezi kufikia maendeleo ambayo inayataka.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Amina Shabani amesema mradi huo utakuwa kichocheo kwa uchumi kwa kuwa ni miundombinu muhimu katika ukuaji wa uchumi.

Desemba mwaka jana Rais John Magufuli alishuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi huo wa umeme kati ya Tanzania na Misri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles