25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Twiga Stars yapania kuichapa Tunisia leo

Na GLORY MLAY- DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya Wanawake nchini ‘Twiga Stars’ inatarajia kushuka dimbani leo dhidi ya Tunisia, katika mchezo wa mashindano ya Mashirikisho ya Soka ya Nchi za Kaskazini mwa Afrika (UNAF), yanayofanyika nchini Tunisia.

Michuano hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na hadi sasa nchi 53 ni wanachama. Tanzania itashiriki michuano hiyo ikiwa nchi mwalikwa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, kwa njia ya simu kutoka Tunisia, kocha mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime, alisema kikosi kipo fiti na leo (jana) walifanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Alisema utakuwa mchezo mgumu lakini wamejipanga kukabiliana na wapinzani wao ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

“Tupo tayari na tunajua mchezo utakuwa mgumu na waushindani, lakini vijana wangu wapo fiti kupambana, tunaomba watanzania waendelee kutuombea ili tukamilishe vyema majukumu yetu yaliotuleta,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles