28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tuzo za Sinema Zetu 2019 kuweka historia mpya

BRIGHITER MASAKI

TAYARI filamu na waigizaji wanaowania tuzo za Sinema Zetu International Film Festival, (SZIFF 2019), wametangazwa huku tuzo zikitarajia kutolewa Februari 23 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Filamu ndefu, fupi, tamthilia na makala zaidi ya 237, zilionyeshwa katika chaneli ya Sinema Zetu na vikapatikana vipengele vya tuzo 30.

Lengo kubwa la tuzo za SZIFF ni kutambua mchango wa wasanii,wazalishaji na wadau wanaofanya vizuri kwenye tasnia hiyo ili kutoa hamasa waigizaji kuzalisha filamu bora.

Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando,  amesema  kuwa SZIFF kwa mwaka huu zimegawanyika katika makundi makubwa mawili ya Swahili Panorama na World Cinema.

Mhando anasema katika kuziweka karibu tuzo hizo na watazamaji, kuna vipengele  kadhaa vimeongezwa ambavyo ni Tamthilia Bora, Mwongozaji Bora, Mwandishi Bora, Mhariri Bora wa Picha Jongevu.

Aidha kuna kipengele kipya cha World Cinama ambacho kitahusisha filamu kutoka nchi zaidi 15 za Afrika ambacho kilisajili filamu 33 na zilizobahatika kupita ni 11.

Tido Mhando aliongeza kuwa filamu hizo zimegawanyika katika makundi mawili. Moja ni zile filamu zinazojadiliwa na jopo la majaji na lingine ni filamu ambazo waigizaji wake wamechaguliwa na mashabiki kupitia kupigiwa kura kwenye tovuti na meseji.

 “Kila mtu anatakiwa kujua kuwa kwa sasa Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi kubwa kuzungumzwa barani Afrika, hivyo tumeamua kufanya tamasha la tuzo hizi ili iwe njia moja ya kufikisha lugha ya Kiswahili kwa watumiaji wapya,

“Kwani tuzo hizo zitashindanisha takribani mataifa yote ya Afrika ambayo yamekubali kushiriki nasi,” anasema Mhando.

Naye mratibu wa tuzo hizo ambazo mlezi wake ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Sophia Mgaza, ameliambia Juma3tata kuwa mwaka huu umekuwa na mafanikio baada ya filamu nyingi kutoka mikoa kushiriki tofauti na mwaka jana ambapo filamu nyingi zilitoka Dar es Salaam.

 “Filamu zilizotangazwa kuingia katika mchuano wa pili ni zile zilizokidhi vigezo na masharti na zimegawanyika katika makundi mawili,

“Kundi la kwanza ni la filamu zote ndefu zilizopatiwa ‘code number’ na kupigiwa kura na watazamaji ambao watapata nafasi yakuchagua Filamu Bora, Mwigizaji Bora,  Kiume na wa Kike na kundi la pili ni filamu zote ambazo zimepitiwa na jopo la majaji na kundi la tatu linajumuisha  filamu zote ambazo zimesajiliwa katika tuzo za Sinema Zetu,” anasema Sophia.

Aliongeza kuwa: “Ni matarajio yetu kuwa tamasha litasaidia kukuza taaluma ya filamu na kuongeza ubunifu na kutambua vipaji na ufanisi uliopo katika tasnia na kuongeza hamasa kwa watazamaji wa filamu za Kiswahili.”

Mwenyekiti wa jopo la majaji Profesa Martini Mhando, anasema upatikanaji wa washiriki katika kila vipengele mbalimbali ulizingatia vigezo vingi hivyo baada ya mchujo filamu zilizopita zina viwango na ubora wa juu.

Miongoni mwa waliotajwa katika mchuano wa vipengele tofauti tofauti ni pamoja na Mwigizaji  Bora wa Kike ambao ni Monalisa, Asha Yasini, Zaudia, Jenifa Temu, Sasha, Johari na Wema Sepetu.

Mwigizaji Bora wa Kiume  ni Mack Dini, Peter Paul, Salum Mpoyoka, Rashidi Msigala, Gabo, Madebe, Mau, Hemed.

Tamthilia zilizoingia ni Talaka, Safari Yangu, Uchawi wa Kizungu,Wagonga Ulimbo.

Uwasilishaji wa kazi hizo ulianza tangu Oktoba Mosi mpaka Novemba 30 mwaka huu. Mchakato wote wa upokeaji wa kazi za wasanii utakuwa chini ya COSOTA na Bodi ya Filamu Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles