23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tunasubiri kuona  maajabu ya LeBrown  kesho

warriorsNew York, Marekani

TAYARI kimenuka. Ndivyo unaweza kusema baada ya timu ya Golden State Warriors kuichapa Cleveland Cavaliers pointi 104-89 katika mchezo wa  fainali ya Ligi ya Kikapu ya Marekani ‘NBA’ iliyochezwa jana uwanja Warriors ‘Oracle Arena uliopo Oakland, Marekani.

James alishuhudia timu yake ikichapwa vibaya na washambuliaji wa Warriors kama vile Stephen Curry, Klay Thompson, Shaun Livingston, Andre Iguodala na Leandro Barbosa aliyemaliza kwa pointi 15.

Kwenye mchezo wa marudiano msimu uliopita Warriors ilishinda ubingwa huo dhidi ya Cavaliers kwenye michezo sita.

Katika mchezo huo Stephen Curry alifunga pointi 11, huku nyota  wa Cleveland, LeBron akimpita kwa kufunga pointi 23 na Kyle Irving ambaye alikuwa na pointi 26 nyingi zaidi ya wengine kwenye fainali hiyo.

Kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Cleveland kesho unaweza  kuwa mgumu zaidi licha ya timu hiyo kufungwa pointi 104-89.

Bado ubora wa washambuliaji wa timu hizo mbili bora kutoka Ukanda wa Mashariki na Magharibi unaweza kuamua fainali hiyo kutokana na kila moja kuwa na mchezaji bora wa NBA.

Mwaka uliopita timu hizo zilikutakana ambapo Golden State iliibuka bingwa kwa uwiano wa 4-2 huku kukiwa na manjonjo kwa nyota wa timu hiyo.

Lakini uzuri wa mchezo huo ni vita iliyopo kati ya Stephen Curry na LeBron James ambapo wote wanatoka mji wa Akron, Ohio pia wamepata mafanikio baada ya kupitia hali ngumu lakini ni wachezaji wa aina tofauti.

Curry amefanikiwa kuwa MVP  mara mbili, ubora wake msimu huu ulimfanya kutengeneza histori na kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya Maurice Podoloff katika kampeni ambayo timu yake pia ilivunja rekodi.

Msimu uliopita mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alisaidia timu yake kushinda uwiano wa 73-9 na kuweka rekodi inayofanana na  Chicago Bull ya 72-10 ya msimu wa  1995-96 ikiongozwa na Michael Jordan.

Katika mchezo huo Curry aliweza kuwa kiongozi mzuri katika mchezo huo ambao alifanikiwa kufunga pointi 30 ikiwa ni uwiano wa asilimia 2 kwa kila mchezo mara ya kwanza kutokea kwa mchezaji wa zamani Allen Iverson mwaka 200-02.

Nyota huyo ambaye hana mwili wa kutisha akiwa na urefu wa futi 6 na nchi 3 amekuwa akiwasumbua sana wachezaji matembo wenye mili mkubwa na walinzi wa timu pinzani

Umahiri wake anapokuwa na mpira licha ya kuwa na mwili mdogo anaweza kufanana na genius wa soka duniani Lionel Messi katika uwiano wa kucheza na akili za wapinzani na kufunga.

Uwezo wa Curry kushinda ni dhahiri kwamba ana kitu maalumu katika mikono yake hasa anapokuwa katika hatua ya mwisho ya umaliziaji.

Hata hivyo huwezi kumdharau LeBron James ‘King James’ ambaye ni mchezaji tofauti sana anayetumia nguvu nyingi kutimiza wajibu wake.

King James (31), ametawala mchezo huo tangu msimu wa 2003 ambapo jana alikuwa katika hali nzuri ya kufanya vizuri katika fainali hiyo.

Wakati Curry akiwa mfalme mpya wa mchezo huo bado mashabiki wanaamini kwamba  hawezi kutamba mbele ya King James kwenye mchezo wa kesho wa mwisho wa fainali hiyo.

Nyota huyo wa Cleveland namba 23 ana uwiano wa pointi 25, rebound 7 na 6 lakini bado hajawa katika kiwango anachotarajiwa alichokionesha katika kila msimu.

Fainali ya jana James aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kucheza fainali sita msululizo katika miaka 50 iliyopita.

Takwimu hii peke yake inaonesha kuwa ujasili na mtu ambaye akati tama ya ushindi awapo uwanjani  pia mchezaji huyo aliingia uwanja wa  Warriors ‘Oracle Arena  baada ya kushinda mfululizo wa michezo 127.

Hata hivyo Cleveland ambayo ilikuwa na wachezaji pacha watatu jana iliingia uwanjani ikiwa na mchezaji mmoja tegemeo baada ya Kevin Love na Kyrie Irving kuwa majeruhi.

Pia Iman Shampert alikuwa na maumizu ya bega hivyo jukumu la kuiongoza timu hiyo katika kunyakua ubingwa liliongozwa na James.

Mfululizo wa mchezo kati ya Warriors na Cavaliers ni wa 14 katika historia ya NBA ambapo safari hii wajilikuta katika fainali.

Timu hiyo iliweza kutetea ubingwa wake kwa uwiano wa 6-7  mwaka  1960  dhidi ya Celtics ikipata ushindi mara nne katika mfululizo wa michezo sita katika fainali hiyo.

Ushindi wa Cleveland ni mara ya kwanza NBA, James alirudi katika mji huo mwaka 2014 ili kuisaidia timu yake kufanikisha ushindi huo.

James alirejea katika timu hiyo ya nyumbani kwao akitokea timu ya Miami Heat ambako alishinda ubingwa wa NBA mara mbili kwa miaka mine aliyocheza.

Mji huo wa Cleveland haukuwahi kushinda ubingwa huo tangu mwaka mashandano hayo yalipokuwa yakiitwa NFL Brwon mwaka

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles