28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

TUME YALIA NA ADHABU YA KIFO

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imeishauri Serikali kufuta adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala  iendane na Azimio la Umoja wa Mataifa.

Taarifa ya Mwenyekiti wa THBUB, Bahame Nyanduga ilisema  azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Na. 62/149 la Desemba 18, 2007 linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuta au kusimamisha utekelezaji wa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala.

“Tunampongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuwafutia adhabu ya kifo wafungwa 61 waliokuwa wakisubiri utekelezaji wa adhabu hiyo katika magereza mbalimbali nchini.

“Uamuzi huo unaendana na azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa namba 62/149 la Disema 18, mwaka 2007,” alisema Nyanduga.

Alisema Tume inatambua kwamba  msamaha huo haufuti adhabu ya kifo katika sheria za nchini hivyo inaishauri serikali kuangalia uwezekano wa kufuta adhabu hiyo.

Nyanduga alisema Tume hiyo inaisihi Serikali, hususan Idara ya Ustawi wa Jamii na wananchi kwa ujumla, kuwapokea na  kuwasaidia  wote waliopewa msamaha  waweze kuendelea na maisha yao kama raia wema katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles