31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tume ya Ushindani yaonya wanaoficha, kupandisha bei vifaa vya kujikinga na corona

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Tume ya Ushindani nchini (FCC), imewaonya waingizaji, wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa jumla na rejareja wa bidhaa za kujikinga na vizrusi vya corona vikiwamo barakoa (mask), vitakasa mikono (sanitizer) na vizuia mikono (gloves) wanaoficha bidhaa hizo kwa lengo la kupandisha bei.

Aidha, imewataka wanaojihusisha na vitendo hivyo ambavyo vimelalamikiwa kuacha mara moja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Alhamisi Machi 19 na Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo, baada ya serikali kutangaza kuwa virusi vya corona vimeingia nchini na kutolewa kwa miongozo ya namna ya kujikinga na maambukizi, wananchi wamejitokeza kwa wingi kununua bidhaa za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo.

Amesema tume imepokea malalamiko juu ya uhaba na kuongezeka kwa kasi kwa bei za bidhaa hizo.

Ametaja bidhaa zinazolalamikiwa ni pamoja na dawa za kutakasa mikono na maeneo yanayoweza kuguswa kwa mikono (Hand Sanitizers and Surface Disinfectants), barakoa (face masks) na vizuizi vya mikono (gloves).

“Tume imefanya uchunguzi wa awali na kubaini uhaba wa bidhaa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona na kwamba maduka kadhaa yamekuwa yakiuza bidhaa hizo kwa bei za juu ilikinganishwa na bei zilizokuwepo kabla ya tangazo la virusi hivyo kuingia nchini.

“Mwenendo huu wa soko unaashiria ukiukwaji wa Sheria ya Ushindani, hususani kupanga bei baina ya washindani, kuficha, kupunguza, au kukataa kusambaza sokoni bidhaa kwa lengo la kupandisha bei na kujipatia faida kubwa isivyo halali,” amesema.

“Vitendo hadaifu dhidi ya walaji wa bidhaa kuhusiana na uhalisia na usahihi wa aina ya bidhaa, tume inawakumbusha walaji kuwa makini katika kununua bidhaa hizo, ikiwa ni pamoja na kukagua bidhaa na kujiridhisha kabla ya kuzinunua, kudai na kutunza risiti za manunuzi na wananchi wenye taarifa kuhusiana na uwepo wa vitendo hivyo sokoni watoe taarifa kwa tume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles