Imechapishwa: Tue, Oct 31st, 2017

TUHUMA NNE ZA ZITTO

Baada ya kuachiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe alikoshikiliwa kwa zaidi ya saa tatu kwa mahojiano na kuhamishiwa katika Kituo cha Kamata, Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Kifedha, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe katika mahojiano ameongezewa makosa mawili.

Kutokana na hali hiyo, hadi sasa anatuhumiwa kuwa na makosa manne pamoja na yale aliyohojiwa katika Kituo cha Chang’ombe ya uchochezi kwa kuwakataza wananchi wasiichague CCM kutokana na Serikali kushindwa kuwakamata waliompiga risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kushindwa kujua chanzo cha maiti mbalimbali zinazookotwa katika ufukwe wa Coco Beach.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Sahibu imesema katika mahojiano hayo Zitto amedaiwa kuchapisha takwimu kinyume na Kifungu cha 37(5) ya Sheria ya Takwimu 2015, kosa analodaiwa kulitenda kwa kusoma taarifa ya Kamati Kuu ya ACT -Wazalendo ambayo ilifanya kwa kina uchambuzi wa takwimu za Serikali juu ya hali ya uchumi wa nchi kusinyaa ambayo tafsiri yake ni kuchapisha takwimu.

Kosa jingine ni kusambaza taarifa hiyo ya Uchambuzi ya Takwimu ya Kamati Kuu ya ACT Wazalendo kwenye mitandao ya Kijamii kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mitandao ya Kijamii (Cyber Crime Act).

 

 

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

TUHUMA NNE ZA ZITTO