30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TUCTA YAMJIBU MSEMAJI WA SERIKALI

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), limelaani kauli ya Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi kuhusu hoja ya Rais kutopandisha mishahara ya watumishi wa umma, ambayo pia alidai ilipotoshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Pia limesema halitaki malumbano na serikali na badala yake wanataka kushirikiana katika kutatua changamoto za wafanyakazi nchini ikiwamo kulipwa malimbikizo ya wafanyakazi.

Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya amesema hayo leo, Oktoba 19 alipokuwa akizungumza na waandishi kuhusu kauli iliyotolewa hivi karibuni na Dk. Abbasi, kutaka umma kupuuza madai halali ya wafanyakazi yaliyowasilishwa kwa serikali katika kikao cha kamati ya utendaji Oktoba 11, mwaka huu.

“Tucta inalaani vikali kauli ya Msemaji wa Serikal kwa kutuhusisha na vyama vya siasa, ifahamike kuwa vyama vya siasa vina lengo la msingi la kuundwa kwake ambalo ni kushika dola na vyama vya wafanyakazi vimelenga kulinda ajira na kuboresha maslahi bora ya wafanyakazi nchini.

“Msemaji huyo anapaswa kufahamu kuwa katiba za vyama vyote vya wafanyakazi nchini ikiwa ni pamoja na ya Tucta hazifungamani na mlengo wowote wa vyama vya siasa nchini kwa kuwa vinafanya kazi kwa kuzingatia miongozo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tumesikitishwa na kitendo cha msemaji huyo kutaka umma kupuuza madai halali ya wafanyakazi tuliyowasilisha na Tucta tunaona kwamba msemaji huyu ama kwa makusudi ya kutokuelewa taarifa yetu na hatuna uhakika kama anaelewa vilivyo majukumu ya msingi ya vyama vya wafanyakazi nchini,” amesema Nyamhokya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles