24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tshisekedi kuapishwa rasmi wiki hii


Kinshasa, Congo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inajiandaa kumwapisha Felix Tshisekedi, kuwa rais mpya wa taifa hilo.

Sherehe za kuapishwa zinatarajiwa kufanyika Alhamisi, wiki hii na zitashuhudiwa Tshisekedi, akiapishwa kuwa rais akichukua mikoba ya Joseph Kabila, aliyeitawala Congo, tangu mwaka 2001.

Awali sherehe hizo zilikuwa zifanyike leo Jumanne, lakini Msemaji wa Muungano wa Upinzani (CACH) ambao ulimuunga mkono Tshisekedi, alisema uwezekano wa kuapishwa ni Alhamisi.

Mahakama ya katiba ilitupilia mbali madai ya mgombea aliyeshika nafasi ya pili Martin Fayulu, na kumthibitisha Tshisekedi, kuwa rais mteule wa Congo.

Tanzania, Burundi na Kenya ni miongoni mwa Mataifa kadhaa ya Afrika yaliyompongeza Tshisekedi,  ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles