22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

TSF YAANZA DORIA ZA ANGA KUHIFADHI MISITU


Na Aziza Masoud, Dar es Salaa

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanza kutumia safari za anga kufanya doria ili kukabiliana na changamoto inayoikabili Serikali katika uhifadhi wa sekta ya misitu na maliasili.

Doria hiyo ilianza jana kwa kuangalia  misitu 10 ya Kanda ya Mashariki iliyopo katika wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga na watalaamu walibaini mambo kadhaa yanayofanyika kinyume na utaratibu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mtendaji Mkuu wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo, alisema lengo la doria hizo ni kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya misitu wanayoilinda.

“Nimetoa maelekezo kwa watendaji wangu kufanya doria ya anga kuanzia leo (jana) na tutaanza na Kanda ya Mashariki, nizitake kanda nyingine zijipange ili kuyabaini  maeneo/misitu korofi kwa kutafuta ramani zake nitawatumia ndege kwa ajili ya doria kutambua uharibifu,” alisema.

Profesa Silayo alisema doria ya misitu imekuwa ngumu kutokana na wahusika kushindwa kuyafikia maeneo yote lakini kupitia doria za anga sasa TFS watapata  nafasi ya kujua kila kinachoendelea katika maeneo yanayowahusu kutumia vikosi kazi vya ulinzi.

Alisema ili kuongeza tija katika doria hiyo TFS itashirikiana na wakuu wa wilaya na wataalamu wa ardhi wa maeneo husika.

Akizungumza baada ya doria hiyo Meneja Msaidizi wa TFS Kanda ya Mashariki, Bernadetha Kadala, alisema doria hiyo imewawezesha kuona kwa karibu zaidi hali halisi ya misitu iliyopo katika kanda hiyo na kufahamu kuna nini kinachotokea kwa wakati huo na itawawezesha kufanya ulinzi kwa weledi.

“Tumeangalia misitu kumi iliyopo Rufiji, Kibiti na Mkuranga na tumeweza kubaini mambo kadhaa yanayofanyika kinyume na taratibu na tumechukua kodineti zitakazotuwezesha kufika moja kwa moja katika eneo husika kwa hatua zaidi,” alisema.

Kadala aliitaja misitu hiyo kuwa ni Mohoro River, Mohoro, Tamburua, Namakutwa/Namueti, Kuchi Hills, Kiwengoma na Utete kutoka Rufiji huku misitu ya Kibiti ikiwa ni Rufiji Delta na Mchungu na Wilaya ya Mkuranga walitembelea Msitu wa Masanganya.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles