27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP AZUNGUMZIA FURSA YA AMANI MASHARIKI YA KATI

TEL AVIV, ISRAEL


RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameeleza matumaini ya kupatikana amani Mashariki ya Kati baada ya kuwasili hapa jana.

Trump ambaye alitokea Saudi Arabia alikohudhuria mkutano wa nchi za Kiislamu, anatarajia kutembelea eneo la Palestina leo.

Rais Trump alipata mapokezi ya heshima za kijeshi yakiongozwa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na Rais Reuven Rivlin.

Trump na Netanyahu walitoa hotuba fupi wakati wa sherehe ya mapokezi, kabla ya kusafiri kwa helikopta kuelekea mjini Yerusalem.

Wote wawili walizungumzia suala la amani, huku Netanyahu akiitaja ziara ya Trump kuwa hatua ya kihistoria kuelekea amani na maridhiano.

Trump kwa upande wake alitaja kuwapo kwa fursa adimu ya kupata amani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Rais huyo wa Marekani anatarajiwa kuyatembelea maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa na Israel katika Ukingo wa Magharibi, ambako atafanya mazungumzo na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles