23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP ATOA ONYO LA MWISHO KWA KOREA KASKAZINI

NEW YORK, Marekani


RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametoa onyo la mwisho kwa Korea Kaskazini akisema kuwa kuna kitu kimoja ambacho  kitafanya kazi ili kukabiliana  na nchi hiyo baada ya miaka kadhaa ya muzungumzo.

Rais Trump alitoa kauli hiyo jana kupitia mtandao wake wa twitter akisema kuwa, marais na uongozi wao wamekuwa wakizungumza na Korea Kaskazini kwa miaka 25, lakini jambo hilo  halijafanikiwa.

Nchi hizo zimekuwa kwenye vita vya maneno kufuatia mipango ya nyuklia ya Korea  Kaskazini, huku Marekani ikitaka kusitishwa majaribio ya makombora.

Korea Kaskazini inasema kuwa imefanikiwa kulifanyia jaribio bomu la haidrojeni ambalo linaweza kubebwa na kombora la masafa marefu.

Awali Trump ameonya kuwa Marekani itaiharibu Korea Kaskazini ikiwa itahitajika kujilinda pamoja na washirika wake.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Jumamosi alisifu silaha za nyulia kama kitu cha nguvu kinachoipa nchi yake ulinzi.

Hivi majuzi Korea Kaskazini ilirusha makombora kupitia anga ya Japan na kupuuza vikwazo vya kimataifa na kufanya jaribio lake la sita la  nyulia Septemba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles