27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS TRUMP ATOA MASHARTI MAPYA YA USAFIRI KWA NCHI 6 ZA KIISLAMU

Rais Donald Trump ameweka masharti mapya ya maombi ya Visa kutoka kwa mataifa sita ya Kiislamu pamoja na wakimbizi wote, ambayo yanawataka kuwa na mtu wanaohusiana ama ushirikiano wa kibiashara na Marekani.

Hatua hiyo inayoyahusisha mataifa yalio na Waislamu kama vile Iran, Libya,Somalia,Sudan ,syria na Yemen imeangaziwa katika ujumbe uliotumwa katika balozi zote.

Masharti hayo mapya yalioanza kufanya kazi siku ya Alhamisi yanaelezea mahusiano ya kifamilia kama mzazi, mkeo ama mumeo,mtoto wa kiume ama wa kike.

Masharti hayo ni baada ya mahakama kuu nchini Marekani kuidhinisha kwa muda agizo la rais Trump ambalo lilikosolewa kuwa marufuku kwa Waislamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles