23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP AMMWAGIA SIFA KANYE WEST

NEW YORK, Marekani


RAIS wa Marekani, Donald Trump, amemfagilia rapa mahiri, Kanye West na mkewe, Kim Kardashian kwa uchapakazi wao mzuri katika kusaidia jamii.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka  72, aliwafagilia  mastaa hao juzi baada ya kukutana nao kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa rais wakati wa chakula cha hisani.

“Kwa sasa tunafanya mambo makubwa na  Kanye West, kusema ukweli msanii huyu ana nguvu,” Trump aliwaambia wageni waliohudhuria hafla hiyo ya chakula cha hisani.

“Hata mkewe Kim pia amekuwa akionyesha juhudi za ukweli kusaidia jamii zinazowazunguka,” alisema Trump wakati akiwamwagia sifa nyota hao.

Mapema mwaka huu, Kim (37) pia aliwahi kukutana binafsi na rais huyo  White House, ambapo aliweza kumwombea msamaha mfungwa Alice Marie Johnson ambaye aliwekwa ndani kwa muda mrefu bila msamaha kwa kosa la kujihusisha na dawa za kulevya na akafanikiwa kumchomoa kifungoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles