27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP AIAMBIA URUSI IJIANDAE KWA KIPIGO NCHINI SYRIA

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS Donald Trump, jana asubuhi ameiambia Urusi ijiandae kwa shambulio la Marekani dhidi ya Syria kufuatia shambulio la kemikali linalolaumiwa kufanywa na Serikali ya Rais Bashar al-Assad.

“Urusi imeapa kutungua shambulio lolote au yote ya makombora yatakayoelekezwa Syria. Kama hivyo mjiandae. Hampaswi kushikamana na wauaji watumiao gesi ya sumu kuua watu na kufurahia unyama,” alisema Trump.

Sehemu ya kwanza ya kauli ya Trump ilirejea kauli ya Balozi wa Urusi nchini Lebanon, Alexander Zasypkin, ambaye alitishia kuangusha au kuzamisha ndege au meli za Marekani zitakazoachia makombora.

“Iwapo kuna shambulio litakalofanywa na Wamarekani, basi makombora yataangushwa na hata kurudishwa kule yalikotoka,” Zasypkin aliiambia televisheni ya kundi la wanamgambo wa Hezbollah, Al-Manar TV

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi Urusi, Vladimir Shamanov, alisema Marekani itakabiliana na kipondo kikali ikiendesha shambulio Syria.

Wakati Marekani iliposhambulia kambi ya anga ya Syria kwa tuhuma za kuendesha shambulio la sumu Aprili 2017, ilitumia makombora ya Tomahawk yaliyozinduliwa kutokea meli yake ya kivita.

“Jeshi la Urusi nchini Syria lina mifumo ya kujilinda yenye uwezo wa kutungua makombora ya Tomahawk ya Marekani,” mtaalamu wa mashambulizi ya anga katika Taasisi ya Royal United Services Institute, Justin Bronk, aliliambia jarida la Business Insider.

Lakini kwa mujibu wa Bronk, urushaji wa shehena kubwa ya makombora ya Marekani utauelemea mfumo huo wa ulinzi, ambao haujafanyiwa majaribio kwa mashambulizi halisi.

Lakini Ikulu ya Urusi ilisema inategemea pande zote zitachukua hatua za kutochokozana na kuvuruga zaidi hali ya Syria ambayo tayari imeharibika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles