26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Trump abanwa na aliyekuwa mshauri wake wa usalama

Washington, Marekani

KUVUJA kwa kitabu cha John Bolton akisema Rais Donald Trump alimtaka kusitisha msaada kwa Ukraine hadi itakapomchunguza Makamu wa zamani wa rais nchini Marekani, Joe Biden, kumewafanya baadhi ya maseneta wa Chama cha Republican kuunga mkono hoja ya kumwalika kutoa ushahidi.

Wajumbe wa chama cha Democratic katika kesi inayoendelea dhidi ya Rais Trump kwenye Baraza la Seneti, wamezidisha shinikizo la kutaka Bolton aliyekuwa mshauri mkuu wa rais huyo kuhusu usalama wa taifa, aitishwe kutoa ushahidi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuvuja kwa sehemu ya kitabu alichokiandika Bolton, ambayo anasema alitakiwa na Trump kusitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine, hadi itakapokuwa imeanzisha uchunguzi dhidi ya Biden.

Ufichuzi huo wa Bolton katika kitabu chake ambacho bado hakijazinduliwa rasmi, umebadilisha mahesabu ya mawakili wa Trump ambao walitaka kesi dhidi ya mteja wao ihitimishwe haraka iwezekanavyo.

PIGO KWA HOJA ZA UTETEZI

Madai ya mshauri huyo wa zamani wa masuala ya usalama, yanapinga hoja ya upande wa utetezi, ambao hadi wakati huu unashikilia kuwa hakuna shahidi yeyote ambaye amejitokeza, akieleza kuwa na ujuzi wa moja kwa moja, kwamba Trump alitaka kuufungamanisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine, na nchi hiyo kuwachunguza wapinzani wake.

Trump anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yake, kwa kumshinikiza Rais wa Ukraine kumchunguza makamu wa rais wa zamani Biden, wakati Washington ikiushikilia msaada muhimu kwa nchi hiyo.

Biden anaweza kuwa mpinzani mkuu wa Trump katika uchaguzi wa rais baadaye mwaka huu.

Trump anashitakiwa pia kulizuia Bunge kutekeleza majukumu yake.

WAREPUBLICAN WASHAWISHIWA

Madai ya Bolton ambaye alifukuzwa kazi na Trump baada ya kutofautiana kimtazamo, yamewafanya baadhi ya maseneta wa Chama cha Republican kubadilisha mawazo, na kutafakari kuunga mkono rai ya Wademocrat, kutaka kuwasikiliza mashahidi, ambayo hadi sasa Warepublican wamekuwa wakiipinga vikali.

 Mmoja wa Warepublican hao ni Seneta Mitt Romney, ambaye anasema hayuko peke yake.

”Nadhani Warepublican wengine wanaweza kujiunga na sisi ambao tunaamini tungepaswa kumsikiliza John Bolton.

”Kama wapo mashahidi wengine na nyaraka nyingine, hilo ni suala tofauti, lakini umuhimu wa ushahidi wa Bolton katika kutusaidia kufanya maamuzi unazidi kuwa wa dhahiri,” alisema Romney. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles