30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TRAFIKI PWANI WAKUSANYA MIL 52/- BARABARANI

traffic-jam3

Na GUSTAPHU HAULE, PWANI

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani, Kitengo cha Usalama Barabarani, limekusanya Sh milioni 52 kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani yaliyotokea katika kipindi cha Novemba na Desemba, mwaka huu.

Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Salum Morimori, alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari mjini Kibaha.

Morimori, alisema kuwa Novemba mwaka huu walianza kufanya operesheni maalumu ya kukamata madereva wanaokiuka sheria za barabarani na kufanikiwa kukusanya Sh milioni 51 zilizotokana na faini kwa makosa 1,738 yaliyokamatwa.
Aidha, alisema katika kipindi cha Desemba operesheni hiyo ilifanyika katika maeneo ya Chalinze na kufanikiwa kukamata magari 44 ambayo kati ya hayo madereva saba wamefikishwa mahakamani na wengine kulipa faini ya Sh milioni 1.1.

Morimori, alisema kuwa makosa yanayokamatwa ni pamoja na mwendokasi, ulevi kwa madereva, kupita magari ya mbele sehemu isiyoruhusiwa, ubovu wa magari pamoja na madareva kukosa leseni.

“Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani kimejipanga kudhibiti ajali za barabarani kwa kufanya operesheni maalumu,  hususani katika kuhakikisha kipindi cha sikukuu kinapita bila ajali,” alisema Morimori.

Aliwataka madereva kutii sheria bila shuruti kwa kuzingatia sheria za barabarani na kwamba yeyote atakayekamatwa akiwa amelewa pombe hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles