23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TRA YATANGAZA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU ZA KODI

Na MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetangaza kutoa msamaha, riba na adhabu  hadi asilimia 100 kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi tofauti na asilimia 50 ya awali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa   na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere jana, lengo la msamaha huo ni kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kulipa malimbikizo ya madeni ya msingi kwa awamu ndani ya mwaka 2018/19.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa msamaha wa riba na adhabu utahusu kodi zote zinazotozwa kwa mujibu wa sheria zinazosimamiwa na TRA.

“Msamaha huo unahusu  ushuru wa forodha unaosimamiwa chini ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004, mapato mengine yasiyo ya kodi ambayo TRA imepewa jukumu la  sheria   kuyakusanya.

“Mapato hayo ni kama vile kodi za majengo na ada za matangazo.

“Walipakodi watakaonufaika na utaratibu huu watatakiwa kuwa na sifa zifuatazo; kwanza wawe wamewasilisha ritani za kodi lakini bado wanadaiwa kodi yote au sehemu ya kodi zitokanazo na ritani hizo.

“Hawajawasilisha ritani za kodi na wana madeni ya kodi, ambao walikuwa wanafanya biashara bila kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), namba ya usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VRN) au  usajili mwingine wa kodi kwa mujibu wa sheria zinazosimamiwa na TRA.

“Waliowasilisha pingamizi za kodi kwa Kamishna Mkuu na ambao pingamizi zao bado zinashughulikiwa katika ofisi za TRA na si kwenye mahakama za ikodi.

“Ambao wamewasilisha pingamizi katika mahakama za kodi na mashauri yao bado hayajatolewa uamuzi, ambao wana madeni ya nyuma ya kodi ambayo hayatokani na kesi za jinai za kodi, utakatishaji fedha, usafirishaji wa binadamu au shughuli nyingine haramu,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa habari kamili usikose nakala yako ya gazeti la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles