24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yapata tuzo ya dhahabu

richard-kayomboNA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)  imepata tuzo ya Ufunguo wa Dhahabu kwa mwaka 2016 baada ya utafiti wa upatikanaji wa taarifa kwenye ofisi za umma uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) katika nchi 11 wanachama wa Shirika la Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Akizungumza na MTANZANIA   Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema  mamlaka imepata tuzo hiyo kutokana na ukusanyaji wake wa kazi kwa uwazi kwa umma.

Kayombo alisema kila mwaka  umekuwa  ukifanyika utafiti wa haki ya kupata taarifa na   uliasisiwa  Septemba 28, mwaka 2002 mjini Sofia, Bulgaria kwa lengo la kuona jinsi  wanachi wanavyoweza kupata taarifa za maendeleo yao ama nchi   kuwawezesha kufanya uamuzi sahihi na stahiki juu ya maisha yao na taifa kwa ujumla.

“Utafiti huu pia hutumika kama chombo cha kuwakumbusha walio katika madaraja na ofisi mbalimbali za umma juu ya wajibu wao wa kutumikia umma kwa uwazi na ukweli ili kuleta maendeleo stahiki nchini,” alisema Kayombo.

Alisema taasisi nyingine za umma zilizowahi kuongoza katika utafiti za nyuma tangu kuanza kwa mchakato huo ni Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Sheria na Katiba , Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango, Wizara ya Nishati na Madini na TRA.

Katika hatua nyingine, TRA kupitia Mkoa wa Kodi Ilala mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa elimu ya kodi kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa wa wilaya hiyo kuwawezesha viongozi hao kuuipeleka kwa wananchi wake.

Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Ofisa Huduma na Elimu wa Mkoa wa Kodi Ilala, Zakeo Kowelo alisema  wamejipanga kuhakikisha elimu ya kodi inamfikia kila mwananchi na kwamba wanaamini kuwa viongozi hao wa mtaa wataifikisha kwa wananchi.

“Pamaoja na mafunzo lakini pia tunatarajia kuwa tunatembelea ofisi za watendaji wa mitaa   kubadilishana uzoefu ikiwa ni pamoja na kutengeneza mazingira ya kuweza kukusanya kodi kwa urahisi kutoka kwa wafanyabiashara wa Kariakoo ambao wapo chini yao,” alisema Kowelo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles