33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TRA YANASA SUKARI YA TANZANIA ILIYOBADILISHWA KUWA YA KENYA

NA SHOMARI BINDA


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara imekamata shehena ya sukari kutoka viwanda vya Kagera na Kilombero ikiwa inabadilishiwa kwenye mifuko ya Kiwanda cha Sukari cha Son Sugar cha  i Kenya   iweze kusafirishwa kwenda nchini humo. 

Sukari hiyo ilikamatwa kwenye ghala la mfanyabiasha Maselo Ghati kwenye mpaka wa Sirari.

Mifuko  353 ya sukari kutoka  kiwanda cha Kagera Sugar ilikamatwa ikihamishiwa kwenye mifuko ya kiwanda cha Son Sugar na kupelekwa Kenya.

Meneja wa TRA Mkoa wa Mara, Ernest Nkangaza, alisema operesheni inayoendeshwa na mamlaka hiyo kwa ushirikiano wa wananchi ndiko kulikofanikisha kukamatwa  sukari hiyo.

Alisema katika tukio hilo,   watu 20 walikamatwa pamoja na mmiliki ambao wanaendelea kuhojiwa na polisi sababu za kuibadilisha sukari ya Tanzania I  ionekane inazalishwa   Kenya wakati kukiwa na changamoto ya uhaba wa sukari na kupanda bei   nchini.

Nkangaza alisema zipo hatua ambazo zitachukuliwa kwa mujibu wa   baada ya taratibu mbalimbali kufuatwa.

Aliwataka  wafanyabishara waache kufanya mambo  kinyume na taratibu kwa kuwa mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wote wasio waaminifu.

"Katika ghala la mfanyabiashara huyu tumekuta pia mifuko tupu ya Kiwanda cha Son Sugar cha   Kenya pamoja na mifuko ya sukari ya Kagera Sugar na Kilombero, jambo ambalo linaonyesha   kuna mchezo mchafu unaofanywa na mfanyabiashara huyu.

"Hili siyo jambo jema hasa ikizingatia kwa sasa kuna shida ya upatikanaji wa sukari na kupanda   bei yake," alisema Nkangaza.

Ofisa Uhamiaji Mfawidhi Kituo cha Sirari, Estom Urio, amesema ni vema kukitumia vizuri kituo cha mpaka  Sirari na kama mtu hajui ni vema aombe ushauri  kwa kuwa hakuna gharama zozote  kufanya biashara kwa uhuru.

Aliwashauri   wafanyabiashara waache kufanya biashara zao kwa njia zisizofaa kwa kuwa kwa sasa maofisa wa serikali wanafanya kazi kwa kushirikiana hasa katika maeneo ya mipakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles