TRA YAFUNGA KIWANDA CHA SARUJI KWA KUSHINDWA KULIPA KODI

0
23

Na HADIJA OMARY- LINDI

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Lindi, imekifunga  kiwanda cha saruji cha Kilwa  kinachomilikiwa  na Kampuni ya Lee Bulding Material Ltd, baada ya  kushindwa kulipa kodi.

Meneja wa TRA Mkoa wa Lindi, John  Jofrey, amesema hatua hiyo imekuja baada ya maofisa wa mamlaka hiyo  kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika eneo hilo la kiwanda na kubaini uwepo  kwa deni la shilingi milioni 89.

“Wafanyabiashara hao wamekaidi agizo la Serikali la kutakiwa  kulipa  kodi  ya mali, ukaguzi zuio, VAT na uendelezaji    ufundi stadi jumla  ya shilingi  milioni  89  kati  ya milioni 193 walizokuwa  wanadaiwa tangu  mwaka  2014,” alisema Jofrey.

“Tumewapa maagizo, tumewahamasisha lakini bado wamekaidi agizo letu, uamuzi tuliochukua ni kufunga kiwanda   kipitia  wakala  baada  ya siku  saba taratibu  za  kuuzwa  mali zilizoko kiwandani,” alisema  Jofrey.

Aidha, Jofrey amesema lengo la kufikia hatua hiyo ni kuhimiza wafanyabiashara  kulipa kodi stahiki  kwa wakati badala  ya  kusukumana na  ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kuacha kushindana na Serikali badala yake kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati.

Ismail Ally ni mwakilishi wa Kampuni ya Lee Building Material Kilwa, amekiri kulitambua deni hilo.

Kwa  upande wa dalali wa  TRA  Mchinga  Action  Malt,  Doment  Likome,  alisema  wamepata  idhini  ya  kuzuia mali za kiwanda hicho  mpaka  watakapolipa deni hilo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here