25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC wataka Watanzania wengi kuwekeza gesi asilia

Faraja Masinde -Dar Es Salaam

SEKTA binafsi nchini imeombwa kuwekeza katika gesi asilia nchini ili Watanzania wengi waweze kutumia nishati hiyo.

Wito huo ulitolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio wakati akizungumzia nishati hiyo katika kipindi cha ‘Dakika 45’ kinachorushwa na kituo cha ITV.

Dk. Mataragio alisema umefika wakati sekta binafsi na Watanzania kwa ujumla kuwekeza eneo hilo.

 “Awali tulikuwa tukifanya huduma hii ya kuweka mifumo ya gesi majumbani na kwenye magari, sasa tunataka watu wa sekta binafsi waje washiriki kuwekeza kwenye eneo hili kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanafikiwa na huduma hii ya nishati.

“Lakini pia tunawahitaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa vituo vidogo vya ujazaji gesi asilia kwenye magari, hatua ambayo mwitikio wake umekuwa ni mkubwa kwani hadi sasa tuna kampuni 24,” alisema Dk. Mataragio.

Alisema Tanzania inatarajia kunufaika zaidi na nishati hiyo kwa kuwa tayari kumeanza kuwa na dalili njema kwenye mapato yanayokusanywa.

“Kuanzia mwaka 2004 hadi 2023/24 tunatarajia kukusanya zaidi ya Sh bilioni 600 kwa ajili ya kodi tu, pia kuna hela ambayo inakwenda kwenye Mfuko wa Mafuta na Gesi Sh bilioni 135 kwa kipindi kifupi.

“Bado tuna futi za ujazo trilioni 57.54 ambazo ziko baharini na hatujaanza kuzivuna, hivyo iwapo tutaanza kuzivuna na kuziuza, mapato ya mafuta na gesi yatainufaisha Tanzania kwa kiwango cha juu sana,” alisema Dk. Mataragio.

Akizungumzia mchangamo wa nishati ya gesi kwenye umeme nchini, alisema imesaidia kuokoa kiwango cha juu cha fedha.

“Tunashukuru kwa sasa tuna umeme wa uhakika bila kuzingatia ni kiangazi au masika, tokea tumeanza kutumia gesi asilia kwenye umeme, kumekuwa na manufaa makubwa kwa nchi kwani tumeokoa kiasi kikubwa cha fedha.

“Kuanzia 2004 hadi sasa tumeokoa kiasi cha dola bilioni 14 sawa na Sh trilioni 32 ambazo ni sawa na bajeti ya nchi kwa mwaka mzima, zilizokuwa zinaigharimu Serikali kwenye matumizi ya umeme, hivyo kumeendelea kuwa na manufaa makubwa kwa uwepo wa gesi,” alisema Dk. Mataragio.

Kuhusu gharama za kufunga mifumo ya gesi kwenye magari, Dk. Mataragio alisema; “tuna uhakika sekta hii ikikua na tukawa na uhakika wa vituo vya gesi nchi nzima. “Hakuna shaka kwamba tutaweza kuwa na gharama rafiki hatua mbayo itachangia Watanzania kuagiza magari yenye mifumo ya gesi moja kwa moja

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles