23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TPA yapata mwarobaini wa Bandari bubu

MWANDISHI WETU-MWANZA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),  Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kuwa mikakati iyoendelea sasa ni kuimarisha sekta ya bandari huku wakipanda kudhibiti bandari bubu zaidi ya 600 kwa sasa.

Hayo ameyasema leo jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa ya utendaji na kuimarika kwa shughuli za Bandari katika Ziwa Victoria.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kuhakikisha wanachukua hatua ikiwamo kuzirasimisha bandari bubu zote ili ziweze kutambulika kwa mujibu wa sheria.

Amesema hiyo ni moja ya changamoto wanayokabiliana nayo TPA ingawa katika kipindi kifupi kijacho wataidhibiti ikiwamo katika Bahari Kuu na Maziwa Makuu nchini.

Amesema wamedhamiria katika kipindi kifupi kijacho zianze kuingiza mapato ya Serikali kwa kuzingiza kwenye mfumo wa malipo wa POS kama njia ya kudhibiti mapato ya Serikali huku wakipanga kufanya mazungumzo na wanaomiliki bandari katika ukanda wa Ziwa ili watambue wajibu wa mamlaka hiyo kama sheria inavyoelekeza.

“Katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dk. John  Magufuli sisi kwetu TPA tumekuwa na mafanikio kadhaa ikiwamo suala la ongozeko la ukusanyaji wa mapato na kufikia Shilingi bilioni 940 huku mkakati wetu ni kukusanya Shilingi trilioni 1.4 kwa mwaka huu wa fedha,” amesema Kakoko

Amesema licha kuwa na mafanikio makubwa ambayo wanajivunia, bado ni wajibu wao kuendelea kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya changamoto ikiwemo hiyo ya uwepo wa bandari bubu.

“Awali kulikuwa na bandari bubu 437 lakini baada ya muda kidogo tukabaini zimeongezeka tena hadi kufikia bandari bubu 601. Mkakati wetu ni kuhakikisha hakuna bandari bubu hata moja ndani ya nchi yetu, na huo ububu hautakuwepo bali ziwe na ndimi ya kutoa fedha kwa manufaa ya Watanzania wote.

“Kuwa na bandari bubu ni ngumu kujua kitu gani kinasafirishwa kupitia bandari hizo , hivyo kiusalama nayo sio jambo nzuri, lazima tufahamu kila kinachoingia na kutoka ndani ya bahari zetu.Tutaweka utaratibu maalumu wa kuzitambua bandari zote bubu na kimsingi tayari tunazifahamu na muda mchache ujao zote zitakuwa zinatambuliwa na TPA,”amesema Mhandisi Kakoko

Amesema kuwa kama uwepo wa bandari bubu unatokana na gharama kubwa katika bandari zilizopo, hilo ni jambo ambalo linazungumzika kwani TPA haipo kwa ajili ya kutaka faida kubwa zaidi ya kutoa huduma kwa gharama nafuu.

“Ukweli tumejipanga kuzidhibiti zote, kama kuna sababu ya kuwepo kwa bandari hizo tutata kufahamu na kutafuta jibu la pamoja. Kama kwenye bandari zetu gharama ni kubwa, ni jambo ambalo linazungumzika, tuko tayari kupunguza na hatimaye sote tuwe tunatumia bandari zinazotambuliwa na TPA,” amesema Kakoko

Kuhusu mikakati iliyopo katika kuboresha miundombinu katika bandari za maziwa makuu zikiwemo bandari za Ziwa Victoria, Mhandisi Kakoko amesema TPA kwa kushirikiana na wadau ikiwemo Kampuni ya Huduma za Meli na TRC wameendelea na mkakati wa kuboresha bandari hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles